BUKOBA SPORTS

Tuesday, October 9, 2012

ARSENAL YAMUWEKA ZAHA KATIKA RADA ZAKE, KWA AJILI YA NAFASI YA THEO WALCOTT


Klabu ya Arsenal iko katika mchakato wa kutafuta mchezaji atakayeziba pengo la THEO WALCOTT baada ya kuingia katika kinyang’anyiro cha kutafuta saini ya mchezaji wa Crystal Palace WILFRIED ZAHA. Aliyekuwa meneja msaidizi wa Arsenal PAT RICE ambaye bado anafanya kazi na klabu hiyo pamoja na kustaafu katika majira ya kiangazi alikuwa akimfuatilia mchezaji mwenye umri wa miaka 19 katika mchezo ambao timu hiyo ilishinda kwa mabao 4-3 dhidi ya Barnley Jumamosi. Arsenal katika kipindi cha karibuni imekuwa ikituma wapelelezi wake katika michezo ya Palace mahsusi kwa ajili ya kufuatilia kiwango cha Zaha hivyo kuwepo uwezekano mkubwa wa kumyakuwa kinda huyo. ZAHA ambaye thamani yake inafikia kiasi cha paundi milioni 12 anaweza kuwa mchezaji mpya kujiunga na Arsenal kutokea katika ligi za chini kama klabu hiyo ikishindwa kumsainisha WALCOTT mkataba mpya. WALCOTT ambaye mkataba wake umebakia miezi isiyopungua 12 amekataa kusaini mkataba mpya ambao utakuwezesha kulipwa kiasi cha paundi 75,000 kwa wiki ingawa bado wapo katika mazungumzo zaidi kupata muafaka wa sakata hilo.

SUDAN YANYANG'ANYWA ALAMA NA FIFA.
Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA limeinyang’anya ushindi wa mabao 2-0 Sudani iliyopata dhidi ya Zambia katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 kwasababu mmoja wa wachezaji aliyefunga mabao hayo hakuruhusiwa kucheza. Kamati ya nidhamu ya FIFA ilifafanua katika taarifa yake kuwa mchezaji huyo aitwaye SAIF ALI hakuruhusiwa kucheza katika mchezo huo uliochezwa June 2 mwaka huu jijini Khartoum. Zambia walilalamika kuwa ALI alicheza katika mchezo huo pamoja na kuwa na kadi mbili za njano katika michezo miwili tofauti ukiwemo mchezo ambao Zambia iliifunga Sudan katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika uliochezwa Februari mwaka huu. FIFA ilikubaliana na malalamiko hayo ya Zambia baada ya kufanya uchunguzi na kuipa ushindi wa mabao 3-0 na pointi tatu nchi hiyo huku ikilitoza faini Shirikisho la Soka la Sudan ya dola 6,430. Zambia sasa inaongoza katika kundi D ikiwa na alama sita katika michezo miwili waliyocheza na Sudan imedondoka mpaka nafasi ya tatu ikiwa na alama moja, Ghana wako nafasi ya pili wakiwa na alama tatu na Lesotho ni ya mwisho wakiwa na alama moja.



AMBROSINI, NAGATOMO WAFUNGIWA SERIE A.
Kiungo wa AC Milan MASSIMO AMBROSINI na beki wa Inter Milan YUTO NAGATOMO ni miongoni mwa wachezaji sita waliofungiwa mechi na maofisa wa Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A. AMBROSINI hakujumuishwa katika kikosi cha AC Milan ambacho kilifungwa na Inter kwa bao 1-0 Jumapili lakini alifungiwa kutokana na tukio lake la kunyanyuka kutoka benchi la wachezaji wa akiba na kusogea karibu na uwanja kuonyesha hasira zake dhidi ya maamuzi ambayo yalikuwa yamefanywa na mwamuzi wa mchezo huo katika dakika ya 47.
NAGATOMO naye alifungiwa mchezo mmoja kufuatia kuonywa kutokana na mchezo mbaya katika kipindi cha kwanza na baadae alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kuunawa mpira kwa makusudi dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza. Wachezaji wengine waliofungiwa mechi moja ni pamoja na YOHAN BENALOUANE na ALESSANDRO LUCARELLI ambao wote wanacheza katika timu ya Parma mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil ZE EDUARDO ambaye anacheza Siena na Beki wa Torino MATTEO DARMIAN.





FA YAMSAMEHE COLE BAADA YA KUOMBA RADHI.
Beki wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Chelsea, ASHLEY COLE anaweza kuepuka adhabu ya kufungiwa baada ya kumuomba msamaha Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA DAVID BERNSTEIN. COLE mwenye umri wa miaka 31 alikuwa akishitakiwa kufuatia kauli yake ya kuiponda FA kuhusiana na hukumu waliyotoa kwa JOHN TERRY kuhusiana na suala ya ubaguzi wa rangi. BERNSTEIN amesema kuwa mchezaji huyo aliomba radhi siku moja baada ya kutoa kauli hiyo na pia alimuomba radhi wakati alipokutana nae jana usiku kwahiyo haoni haja ya kumchukulia hatua yoyote kwakuwa anajutia alichokifanya. Maamuzi ya kama mchezaji huyo atajumuishwa katika kikosi cha Uingereza katika mchezo wa kufuzu dhidi ya San Marino na Poland yamebakia kwa meneja wa kikosi hicho ROY HODGSON. Akihojiwa kama COLE anaweza kupewa unahodha katika mechi hizo BERNSTEIN alifafanua kuwa FA waliweka wazi toka mwanzo kuwa mchezaji ambaye atakuwa anakiongoza kikosi cha nchi hiyo ni lazima awe na nidhamu ya hali ya juu.


PRINCE WILLIAM NA MKEWE KUFUNGUA KITUA KIKUBWA CHA MICHEZO UINGEREZA.


Wajukuu wa malkia ELIZABETH wa pili wa Uingereza, PRINCE WILLIAM na mkewe KATE MIDDLETON wanatarajiwa kufungua kituo kipya cha michezo kiitwacho St George Park kilichopo Staffordshire. Kituo hicho kilichogharimu paundi milioni 105 ambapo PRINCE WILLIAM atakuwa rais wake kinatarajiwa kuinua kiwango cha soka nchini Uingereza kwa rika zote.Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha nchi hiyo-FA, DAVID BERNSTEIN amesema kuwa matarajio waliyonayo yatawezekana kutokana na kuwapa mafunzo zaidi na bora makocha wa soka ambao watapewa jukumu la kuwafundisha soka vijana wa rika mbalimbali nchini humo. Kituo hicho mbali na kutoa mafunzo kwa makocha lakini pia kitashughulika na mambo ya matibabu ya michezo, sayansi ya michezo pamoja na masuala ya ushauri nasaha. 
PRINCE WILLIAM na mkewe KATE MIDDLETON wakisalimiana na wadau mbalimbaliHapa wakitembelea eneo lenyewe wakiongozwa na katibu mkuu wa FA ndugu Alex na mwenyekiti wa FA ndugu David BernsteinPRINCE WILLIAM na mkewe KATE MIDDLETON wamekutana na timu ya Enland.

No comments:

Post a Comment