BUKOBA SPORTS

Sunday, October 7, 2012

ARSENAL YANG'ARA UGENINI NA KUSHINDA 3-1 DHIDI YA WEST HAM UNITED... CHELSEA YAIUA NORWICH CITY 4-1, MAN CITY YAIKANDAMIZA SUNDERLAND 3-0, WEST BROM 3 2 QPR


Sasa nd'o nimeanza safari ya kufunga mabao kama mvua ... Olivier Giroud wa Arsenal (katikati) akifunga dhidi ya West Ham wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Upton Park leo, Oktoba 6, 2012. (Picha: BBC)

Gooooh...! Fernando Torres akiifungia Chelsea bao la kusawazisha dhidi ya Norwich.

Nahodha Holt wa Norwich akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza dhidi ya Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Oktoba 6, 2012.

Safiiii... Torres wa Chelsea akipongezwa na wachezaji wenzake Juan Mata na Ivanovic baada ya kufunga goli lao la kusawazisha dhidi ya Norwich City leo.

Hazard wa Chelsea akifunga dhidi ya Norwich katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo.

Thomas Vermaelen wa Arsenal (kushoto) akichuana na Andy Carroll wa West Ham wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Oktoba 6, 2012.
LONDON, England
Olivier Giroud alifunga goli lake la kwanza la Ligi Kuu ya England akiwa na Arsenal wakati 'Gunners' wakicharuka kutoka kuwa nyuma na kushinda ugenini kwa mabao 3-1 dhidi ya West Ham jkwenye Uwanja wa Boleyn Ground, Upton Park jijini London usiku huu.

West Ham walipata goli la utangulizi kinyume na mwelekeo wa mechi katika dakika ya 21 wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Sengal, Mohamed Diame alipopiga shuti kali la 'upinde' lililomshinda kipa Vito Mannone na kujaa wavuni.

Giroud alisawazisha kabla ya mapumziko wakati alipoiwahi krosi ya Lukas Podolski na kuiunganishia wavuni, pembeni kwa ndani ya mlingoti wa goli.

Kevin Nolan
alikosa nafasi mbili za wazi kuwapa wenyeji uongozi na aliadhibiwa baada ya Santi Cazorla kuifungia Arsenal bao la pili na mtokea benchi Theo Walcott aliyechukua nafasi ya Gervinho akaongeza goli la tatu wakati Arsenal wakicheza gonga safi huku West Ham wakionekana 'kutepeta'.

Giroud alifunga goli lake la kwanza katika ligi kuu ya England tangu atue Arsenal akitokea Ufaransa mwanzoni mwa msimu huu na kucheza kwa dakika 303 bila mafanikio. Goli hilo lilitokana na shuti lake la 12 (jumla 15, ukichanyanya na yaliyoyozuiwa) tangu aanze kucheza katika ligi kuu ya England.

Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, Man City iliikandamiza Sunderland kwa mabao 3 - 0, Chelsea ikashinda 4-1 dhidi ya Norwich, Swansea na Reading zikatoka sare ya 2 - 2, West Brom wakazidi kuiweka pabaya Queen's Park Rangers kwa kuichapa mabao 3 - 2 na Wigan na Everton pia zikatoka sare ya 2 - 2.

No comments:

Post a Comment