>>LIGI KUU kusimama hadi Oktoba 20 kupisha Mechi za Kimataifa!
Katika Mechi za Ligi Kuu England, BPL,
zilizochezwa jana, Manchester United, wakicheza huko Sports Direct Arena,
waliwatwanga wenyeji wao Newcastle bao 3-0 na kushika nafasi ya pili
wakiwa Pointi 4 nyuma ya vinara Chelsea huku huko Anfield Liverpool
walitoka 0-0 na Stoke City na ndani ya White Hart Lane, Tottenham
wameendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa Aston Villa bao 2-0.
Matokeo:
Jumapili Oktoba 7
Southampton 2 Fulham 2
Tottenham Hotspur 2 Aston Villa 0
Liverpool 0 Stoke City 0
Newcastle United 0 Manchester United 3
Southampton 2 Fulham 2
Kona ya Adam Lallana iliunganishwa na
Jose Fonte na kuandika Bao la kwanza kwa Southampton katika Dakika ya 4
ambalo lilidumu hadi Dakika ya 70 na Fulham kusawazisha kwa bao la
kujifunga mwenyewe Jos Hooiveld baada ya shuti la John Arne Riise
lililokuwa likitoka nje kuguswa na Mchezaji huyo wa Southampton na
kujifunga.
Fulham walipiga bap la pili kupitia
Kieran Richardson katika Dakika ya 90 lakini Southampton walisawazisha
katika Dakika ya 90 kwa bao la pili la Jose Fonte.
VIKOSI:
Southampton: Gazzaniga, Richardson, Yoshida, Fonte, Fox, Puncheon, Schneiderlin, Steven Davis, Lallana, Rodriguez, Lambert
Akiba: Kelvin Davis, Hooiveld, Ward-Prowse, Do Prado, Mayuka, Chaplow, Reeves.
Fulham: Schwarzer, Riether, Hughes, Hangeland, Riise, Kacaniklic, Ruiz, Baird, Sidwell, Duff, Rodallega
Akiba: Stockdale, Kelly, Senderos, Kasami, Karagounis, Richardson, Briggs.
Refa: Mark Clattenburg
Tottenham Hotspur 2 Aston Villa 0
Bao za Kipindi cha Pili za Steven
Caulker, Dakika ya 58, na Aaron Lennon, Dakika ya 67, zimewapa ushindi
wa bao 2-0 Tottenham walipocheza kwao White Hart Lane na Aston Villa.
VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen, Lennon, Dembele, Sandro, Bale, Defoe, Dempsey
Akiba: Friedel, Huddlestone, Adebayor, Dawson, Sigurdsson, Falque, Townsend.
Aston Villa: Guzan, Bennett, Vlaar, Clark, Lowton, Holman, El Ahmadi, Delph, Albrighton, Benteke, Agbonlahor
Akiba: Given, Bent, N'Zogbia, Westwood, Bannan, Weimann, Lichaj.
Refa: Neil Swarbrick
________________________________
________________________________
Liverpool 0 Stoke City 0
SUAREZ AFUNGIWE kwa kujidondosha makusudi!
Ule mwendo wa kusuasua wa Liverpool
kwenye Ligi Kuu umeendelea tena leo baada ya kushindwa kupata ushindi
wakiwa Uwanja wa nyumbani Anfield walipotoka 0-0 na Stoke City
iliyosimama imara kabisa.
SUAREZ AFUNGIWE kwa kujidondosha makusudi!
>>MENEJA STOKE CITY, Pulis, aitaka FA imuadhibu Suarez!!
>>MENEJA mwingine ataka RVP aadhibiwe!!
Bosi
wa Stoke City Tony Pulis amekitaka Chama cha Soka England, FA,
kimuadhibu Straika wa Liverpool Luis Suarez kwa tabia yake ya kutaka
kuwahadaa Marefa kwa kujidondosha makusudi ndani ya boksi ili apate
Penati.
Jana, Stoke City ilikuwa Anfield kucheza
na Liverpool kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo ilimalizika 0-0 na
katika Kpindi cha Pili Luis Suarez ‘alijidondosha’ kutaka Penati ambayo
Tony Pulis anaamini ulikuwa ni udanganyifu.
Pulis amesema: “Siku nyingi nimepigia
kelele hili na Kipindi cha Pili tukio moja lilikuwa aibu kubwa! FA
walitazame hili. Wampe Kifungo Mechi 3 na ataacha kujirusha!”
Alipohojiwa, Meneja wa Liverpool,
Brendan Rodgers, alijibu: “Sikuona tukio hilo hivyo siwezi kusema
chochote lakini chochote anachofanya Luis litakuwa tatizo tu!”
Hata hivyo, kuhusu tukio la Suarez
kujidondosha kwa makusudi, FA haiwezi kuchukua hatua yeyote ile kwani
Sheria zinawaruhusu kutoa adhabu pale tu matukio yalistahili Kadi
Nyekundu na Refa hakuona na si matukio ambayo yangestahili Kadi ya
Njano.
Wakati huo huo, Meneja wa Newcastle
United Alan Pardew ameitaka FA imwadhibu Straika wa Manchester United
Robin van Persie kwa kile alichodai kumpiga ‘kipepsi’ Kiungo wa
Newcastle, Yohan Cabaye, katika Mechi ya jana ya Ligi Kuu England huko
Sports Direct Arena ambayo Manchester United iliitandika Newcastle bao
3-0.
Ingawa mwenyewe amekiri hakuliona tukio
ambalo lilitokea wakati si Van Persie wala Cabaye kuwa na mpira huku
wote wakikimbilia golini, Pardew amedai: “Van Persie alimtazama Cabaye
na kumpiga kiwiko, nikiwa mkweli, FA walitazame tukio hilo.”
FA inaweza kulipitia tukio hilo na kutoa
adhabu ikiwa tu Refa wa Mechi hiyo, Howard Webb, atakiri hakuliona
tukio hilo na kama angeliliona angetoa Kadi Nyekundu.
VIKOSI:
Liverpool: Reina, Wisdom, Skrtel, Agger, Johnson, Gerrard, Allen, Sahin, Fernandez Saez, Suarez, Sterling
Akiba: Jones, Henderson, Cole, Assaidi, Coates, Carragher, Borini.
Stoke: Begovic, Cameron, Huth, Shawcross, Wilson, Walters, Nzonzi, Whelan, Adam, Kightly, Crouch
Akiba: Sorensen, Jones, Edu, Whitehead, Upson, Etherington, Jerome.
Refa: Lee Mason
Newcastle United 3 Manchester United 0
Bao za Johnny Evans, Dakika ya 8,
Patrice Evra, Dakika ya 16 na Tom Cleverly, Dakika ya 71, yamewapa
ushindi Manchester United wa bao 3-0 dhidi ya Newcastle.
Bao la Cleverly, bila shaka, litaingia katika ile Listi ya Mabao Bora ya Msimu.
VIKOSI:
Newcastle United: Harper; Santon, Williamson, Perch, Ferguson; Ben Arfa, Tioté, Cabaye, Gutiérrez; Ba, Cissé
Akiba: Alnwick, Simpson, Anita, Bigirimana, Obertan, Sammy Ameobi, Shola Ameobi
Manchester United: De Gea; Rafael, Ferdinand, Evans, Evra; Carrick, Cleverley; Kagawa, Rooney, van Persie, Welbeck
Akiba: Lindegaard, Scholes, Valencia, Anderson, Giggs, Hernandez, Wootton.
Refa: Howard Webb
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Oktoba 20
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Tottenham v Chelsea
[Saa 11 Jioni]
Fulham v Aston Villa
Liverpool v Reading
Man United v Stoke City
Swansea v Wigan
West Brom v Man City
West Ham v Southampton
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Norwich v Arsenal
Jumapili Oktoba 21
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Sunderland v Newcastle
[Saa 12 Jioni]
QPR v Everton
No comments:
Post a Comment