MECHI YAWEKA REKODI: KADI za NJANO 8 Mechi moja Timu moja!
West Ham wamezidi kumletetea mchecheto
Meneja wa Queens Park Rangers Mark Hughes wakati jana walipotua nyumbani
kwao Loftus Road na kuwatandika bao 2-1 na kuwaacha wakimaliza Mechi
hiyo wako Mtu 10 na pia kuendelea kubaki mkiani mwa Msimamo wa Ligi Kuu
England baada ya kuambulia Pointi mbili tu katika Mechi 6.
KADI ZA KIHISTORIA
• West Ham ndio Timu ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kupata Kadi za Njano 8 katika Mechi moja.
• QPR wamezoa jumla ya Kadi Nyekundu 10 tangu mwanzo mwa Msimu wa 2011-12 ambazo ni Kadi 3 zaidi ya Timu nyingine yeyote.
West Ham walianza vyema na kupata bao
katika Dakika ya 3 tu alilofunga Matt Jarvis na Ricardo Vaz Te akapiga
bao la pili kabla ya mapumziko.
MAGOLI:
QPR 1
-Taarabt 57′
WEST HAM 2
-Jarvis 3′
-Vaz Te 35′
Baada ya mapumziko, QPR wakazinduka na
kukaza buti hasa baada ya kuwaingiza Adel Taarabt na Samba Diakite, na
Taarabt ndie alieipa QPR bao lao moja kwa shuti kali na zuri.
Hata hivyo, QPR walipata dosari pale Samba Diakite alipobandikwa Kadi za Njano mfululizo na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Ushindi huu umewapaisha West Ham hadi
nafasi ya 7 na kuleta faraja kwa Meneja Sam Allardyce ambae pia
alifurahi kurudi Uwanjani kwa Straika wake mpya wa mkopo kutoka
Liverpool, Andy Carroll, ambae alumia katika Mechi yake ya kwanzakuichezea West Ham na jana alimudu kucheza Dakika 20 za mwisho.
VIKOSI
Queens Park Rangers:
Julio Cesar, Hill, Onuoha (Hoilett - 84' ), Nelsen, Park Ji-sung
(Diakite - 55' ), Wright-Phillips (Taarabt - 56' ), Granero, Faurlin,
M'bia, Cisse, Zamora
Akiba: Green, Diakite, Taarabt, Ephraim, Ehmer, Mackie, Hoilett
West Ham United:
Jaaskelainen, Reid (Tomkins - 23' ), O'Brien (McCartney - 35' ),
Collins, Demel, Nolan, Jarvis, Noble, Diame, Cole, (Carroll - 72' ), Vaz
Te
Akiba: Henderson, McCartney, Tomkins, Benayoun, O'Neil, Carroll, 11 Maiga
Refa: Clattenburg
Watazamaji: 17,363
No comments:
Post a Comment