Mchezaji Papa Bouba Diop
Birmingham City imesaini mkataba wa muda mfupi na mchezaji Papa Bouba Diop.
Baada ya kufanya mazoezi na timu ya Chelsea kwa
wiki kadhaa zilizopita, mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye
umri wa miaka 34 amefaulu katika vipimo vya afya na atatia saini mkataba
wa mwezi mmoja, wakati maombi ya visa yake yakisubiriwa.
Diop alijenga jina lake katika soka la England baada ya kujiunga na Fulham akitokea timu ya Lens ya Ufaransa mwaka 2004.
Aliichezea timu hiyo kwa misimu mitatu akiwa na Fulham, ambako alicheza pamoja na boss wa Chelsea, Lee Clark.
Baada ya hapo alihamia timu ya Portsmouth mwaka 2008, ambako alishinda kombe la FA katika msimu wake wa kwanza katika timu hiyo.
Akiwa amenyakua kombe la Ugiriki mwaka 2011
akiichezea timu ya AEK Athens, alirejea England msimu uliopita akijiunga
na West Ham.
Aliichezea timu hiyo mara 16 lakini baada ya
Desemba hakupatiwa nafasi kubwa ya kuichezea timu hiyo na kuachwa msimu
huu wa majira ya joto.
Diop aliiwakilisha Senegal mara nne katika
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na kuwa miongoni mwa wachezaji wa
timu hiyo iliyofikia hatua ya robo fainali katika fainali za Kombe la
Dunia za mwaka 2002, zilizoandaliwa kwa pamoja kati ya Japan na Korea
Kusini.
No comments:
Post a Comment