Madam Ritha akitoa maoni yake juu ya mshiriki aliyekua juu ya jukwaa Jumapili ya tarehe 15, October 2012 mshiriki mmoja wa EBSS, Linias Mhayaaliyaaga mashindano na hivyo kubaki washiriki tisa tu. Washiriki tisa waliobakia wamegawanywa katika makundi matatu na kila Jaji kapewa washiriki
watatu watakaokuwa chini ya usimamizi wake, majaji wanatakiwa kuwapa maelekezo kuhusu kuimba na kuwachagulia nyimbo za kuimba.
Godfrey Kato akiingia katika jukwaa
Husna Nassor akiimba jukwaani
Menynah Atick akiimba mbele ya majaji na watazamaji

Salma Yusuph akipiga gitaa
SAFARI YA LINIAS KUTIMIZA NDOTO ZAKE ILIANZIA TUSKER PROJECT FAME 5 HUKO NAIROBI
Linias aliondoka Mwanza tarehe 26 April,2012 na kuelekea Dar es salaam
kwenye Audition za Tusker Project Fame 5 zilizofanyika kesho
yake(tarehe 27-28). Akawa miongoni mwa watanzania 4 tu waliochaguliwa
kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo. Tarehe 18 May akatua Nairobi
tayari kwa shughuli hiyo.
.
Tarehe 19 may, Audition za Top 25 zikafanyika, washiriki 7 akiwemo
mtanzania 1 walirudi makwao. washiriki 6 akiwamo Linias wakawekwa kwenye
Probation na ilitakiwa waimbe jukwaani siku ya ufunguzi wa mashindano
hayo wiki mbili baadaye ili kupata nafasi ya watu 3 kuingia kwenye
Academy. Washiriki hao ni Doreen(kenya), Joe(Burundi), Nancy(sudan
kusini), Linias(Tanzania), Brian(Uganda) na Diana(Rwanda). Linias
alichaguliwa wimbo wa Mbagala wa msanii Diamond.

Kwa kuzingatia kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kwa kijana huyo kuimba
jukwaani na mbele ya mamilioni ya watazamaji wa Afrika mashariki,
alijitahidi kadri ya uwezo wake kutoa kile alichokuwa nacho. Pamoja na
kuimba vizuri, bado Linias hakufanikiwa kupata nafasi kati ya hizo 3
zilizokuwa zimebakia, hivyo safari ya Tusker ikawa imeishia usiku huo.
Washiriki waliofanikiwa kuendelea na mashindano ni Doreen, Nancy na Joe.
Linias alirejea Tanzania tarehe 4 June mwaka huu na kuelekea Mwanza
kujinoa zaidi kwani haikuwa mwisho wa maisha yake kimuziki.
_____________________________________________________________
WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL WAWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA KUPIGWA PICHA ZA UCHI WAKATI WA TAMASHA LA FIESTA DODOMA.
No comments:
Post a Comment