BUKOBA SPORTS

Monday, October 15, 2012

MENEJA FERDINAND COLY: SENEGAL ITAKUBALI ADHABU ITAKAYOTOLEWA!!

Fans of Ivory Coast help other fans escape the violence in the upper tiers of Leopold Sedar Senghor stadium in Dakar October 13 2012. Senegal's African Nations Cup tie with Ivory Coast was abandoned on Saturday when riot police fired teargas inside the packed stadium as thousands of fans lit fires and threw objects in protest at the home team's poor performance. The fans are being lowered as rocks were being thrown towards the upper tiers.

MENEJA wa timu ya taifa ya Senegal, Ferdinand Coly amesema kuwa timu yake itapkea adhabu yoyote watakayopewa kwa ajili ya vurugu zilizotokea katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Ivory Coast. Katika mchezo huo wacheza na mashabiki wa Ivory Coast walirushiwa mawe, chupa na viti na mashabiki wenye hasira wa Senegal wakati wa mchezo wa Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Leopold Sedar baada ya ya wageni kuongoza kwa mabao 2-0 zikiwa zimebaki dakika 15 kabla ya mchezo kumalizika. Mara baada ya mashabiki hao kuwasha moto na kuanza kurusha kuelekea uwanjani wachezaji pamoja na mashabiki wapatao 300 wa Ivory Coast walilazimika kupewa ulinzi mkali katikati ya uwanja wakati polisi wakijaribu kurusha mabomu ya machozi kuelekea kwa mashabiki wan chi hiyo waliokuwepo jukwaani. Coly ambaye pia amewahi kuwa mchezaji katika kikosi cha Senegal amesema kuwa anajua watapambana na adhabu kali lakini watakubaliana nayo kutokana na tukio hilo. Vurugu zilianza katika uwanja huo ambao ulikuwa na watu wapatao 60,000 baada ya penati iliyopigwa na nahodha wa Ivory Coast Didier Drogba na kuipa ushindi timu yake wa mabao 2-0 na mchezo huo kuvunjika zikiwa zimebakia dakika 15.Manchester City star Yaya Toure Askari wakijaribu kumkinga.Kolo Tour na yeye kidogo apigwe.
Kimenuka.... Dakar



Mashabiki wa Senegal wakifanya vurugu uwanja wa Leopold Sedar Senghor

No comments:

Post a Comment