






Yanga leo kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wamepigwa bao 1-0 na Kagera Sugar na kuporomoshwa hadi nafasi ya 8
katika Mechi pekee ya Ligi Kuu Vodacom huku ushindi huo ukiupaisha
Kagera Sugar hadi nafasi ya 3 kwa kufikisha Pointi 10 wakiwa nyuma ya
Azam wenye Pointi 13 na vinara Simba wenye 16.
Bao la ushindi kwa Kagera Sugar lilifungwa katika Dakika ya 68 na Themi Felix.
Mechi hii ya Kagera Sugar na Yanga
ilikuwa ichezwe jana lakini kutokana na Uwanja wa Kaitaba kuwa na
shughuli nyingine za kijamii ikaahirishwa hadi leo.
Mechi ifuatayo kwa Yanga ni huko Mwanza dhidi ya Toto Africans Siku ya Alhamisi Oktoba 11.
MSIMAMO:
1 Simba Mechi 6 Pointi 16
2 Azam FC Mechi 5 Pointi 13
3 Kagera Sugar Mechi 6 Pointi 10
4 Prisons Mechi 6 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 1]
5 Coastal Mechi 6 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 0]
6 JKT Oljoro Mechi 6 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 0]
7 Mtibwa Sugar Mechi 5 Pointi 8 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Yanga SC Mechi 6 Pointi 8 [Tofauti ya Magoli 1]
9 Toto African Mechi 6 Pointi 7 [Tofauti ya Magoli 0]
10 Ruvu Shooting Mechi 6 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -2]
11 African Lyon Mechi 6 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -5]
12 JKT Ruvu Mechi 6 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -7]
13 JKT Mgambo Mechi 6 Pointi 3
14 Polisi Moro Mechi 6 Pointi 2



Kocha wa Kagera Abdallah King Kibadeni (kulia) na wasaidizi wake


Bench la Wachezaji wa Kagera Sukari.

Said Bahanuz aliumia na nafasi yake ikachukuliwa Jerson Tegete


Meza kuu



Hadi Half time hakuna timu iliyokuwa imemchungulia mwenzake.



Wapenzi wa soka Jukwaa la Golani maarufu kama Jukwaa la Balimi. wakiangaliwa kwa makini Askari wa Ulinzi uwanjani hapo





Mashabiki

Mashabiki
VIKOSI:
YANGA 1.Yaw Berko 2.Juma Abdul 3.Stephano Mwasika 4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C)5.Mbuyu Twite 6.Athuman Idd 'Chuji' 7.Nizar Khalfan 8.Frank Domayo 9.Said Bahanunzi 10.Didier Kavumbagu 11.Haruna Niyonzima
Akiba:
1.Ally Mustapha 'Barthez'
2.Oscar Joshua
3.Ladislaus Mbogo
4.Omega Seme
5.Shamte Ally
6.Nurdin Bakari
7.Jeryson Tegete
KAGERA SUGAR
1.Andrew Ntalla 2. juma Nade 3. Kanoni Salim 4. Amandus Nnesta 5. Benjamini Effe 6. Malegesi Mwangwa 7. Daudi J'nne 8. George Kavilla 9. Enyinna Darlington 10. Shija Mkiwa 11. Wilfred Ammeh
Akiba:
1. Kalysubula Hannyngton
2. Ally Abdulkareem
3. Laban Kambole
4. Mecky Michael
5. Temi Felix
6. Paul Ngwai
7. Kamana Salum
No comments:
Post a Comment