BUKOBA SPORTS

Saturday, October 13, 2012

PICHA ZA MSIBANI KWA MAREHEMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA RPC LIBERATUS BALLOW , PAMOJA NA SEHEMU WALIYO MUULIA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Everest Ndikillo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tukio la kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberetus Ballow usiku wa Kuamakia leo maeneo ya Kitangiri.

Nyumba ya Dorcas Moses mwalimu wa shule ya Msingi ya Nyamagana ambye alikuwa kwenye gari aina ya Rav 4 aliyepewa lifti na kamanda Ballow usiku kumrudisha kwake. Hapa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Fredrick Katulanda akitoka kufanya mahojiano.

Mtoto wa kaka yake Mwalimu Dorcas akiongea kuhusiana na tukio la Kifo cha kamanda Ballow ambapo yeye ndie alikwenda kufungua geti kwa ajili ya Mama yake Dorcas aweze kuingia ndani ila kabla ya kufungua ndipo aliposikia risasi ikipigwa.

Hapa ni nyumbani kwa marehemu kamanda Ballow.

Hili ndilo geti ambalo kifo cha kamanda Ballow kilipotokea usiku wa kuamkia leo wakati mwalimu Dorcas Mosese alipokuwa akirudi nyumbani kwa lifti ya gari la Kamanda Ballow.

Baadhi ya jamaa yake marehemu nyumbani kama walivyokutwa na kamera yetu.
Kwa picha zaidi bofya read more

No comments:

Post a Comment