BUKOBA SPORTS

Monday, October 15, 2012

SEBASTIAN VETTEL ANYAKUWA TAJI LA DEREVA BORA KOREA GRAND PRIX

Sebastian Vettel wa Red Bull
Sebastian Vettel wa Red Bull ameimarisha matumaini yake ya kunyakuwa taji la dereva bora msimu huu wa mbio za magari ya Langa langa baada ya kuibuka na ushindi katika mashindano ya Korea Grand Prix.
Kufuatia ushindi huo, Vettel sasa ametwaa uongozi wa msururu wa mashindano hayo kutoka kwa Fernando Alonso wa Ferrari.
Huu ni ushindi wa tatu kwa Vettel unaomfanya kuwa dereva wa kwanza kushinda mbio nne katika msimu huu.
Dereva mwenzake Mark Webber alimaliza wa pili akifuatiwa na Alonso. Vettel anaongoza kwa pointi sita dhidi ya Muhispania huyo huku kukiwa na mbio nne zaidi kabla ya msimu kukamilika.
Matumaini ya Muingereza Lewis Hamilton kutwaa taji yamekufa baada ya dereva huyo wa McLaren kumaliza nafasi ya kumi.
Kimi Raikkonen wa Lotus alishika nafasi ya tano na kumuondoa Hamilton katika nafasi ya tatu ya dereva bora.
Vettel ana alama 48 mbele ya Raikkonen, na pia sitini na mbili zaidi ya Hamilton, huku kukiwa na alama mia moja tu ambazo bado zipo katika mashindano yaliyobaki ya nchini India, Abu Dhabi, Marekani na Brazil.

Jenson's front right was burst after colliding with Kobayashi


Vettel led from the first corner to last and now leads the F1 championship


Hamilton endured a torrid afternoon - and was seen dragging astroturf under his car at one stage

... Tumetokelezea...

DADAZ WAKIJIKOSHA KWENYE UKODAK

Gangnam style: Ubiquitous rapper Psy was on hand to teach the drivers his moves

Alonso admitted he had got the best result possible and knows Ferrari need to find more speed if he is to take the fight to Vettel over the final four races.Picha kwa hisani ya mtandao wa Dailymail
 _______________________________________



WATSON NAYE ANYAKUWA TAJI  MICHUANO YA WAZI YA JAPAN.

 MCHEZA tenisi Heather Watson anakuwa mwanadada wa kwanza wa Uingereza kushinda taji la WTA toka mwaka 1988 baada ya kufanikiwa kumfunga Kai-Chen Chang katika mchezo wa fainali ya michuano ya wazi ya Japan. Watson ambaye anashika namba 71 katika orodha za ubora duniani kwa upande wanawake alifanikiwa kumfunga Chang raia wa Taipei ambaye anashika namba 134 kwa seti 2-1 zenye alama za 7-5 5-7 7-6.
Watson pia amefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya wawili wawili akiwa na Kimiko Date-Krumm ambapo watacheza na Abigail Spears na Raquel Kops-Jones wa Marekani.

Ushindi huo wa Watson aliopata jijini Osaka unakuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya mwingireza mwenzake Laura Robson kutinga fainali ya michuano ya wazi ya Guangzhou iliyofanyika China na kuwa mwanamke wa kwanza nchini Uingereza kutinga fainali ya michuano ya WTA toka Jo Durie alipofanya hivyo mwaka 1990.
Watson akibusu kombe

Watson ni mzoefu na ameweza kushinda taji hilo kwa kujiamini

No comments:

Post a Comment