Beki wa Yanga, Stephano Mwasika akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa Simba, Nassoro Masoud 'Cholo' katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara unaoendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Kaseja atika harakati za kukomboa.
YANGA imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na wapinzani wao wa jadi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuanzia saa 1:02 usiku.
Yanga ambao walimaliza mechi hiyo wakiwa pungufu baada ya Simon Msuva kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 77 kwa kumrudishia rafu Juma Nyosso, ndio waliohaha kusawazisha bao, baada ya kutanguliwa kwa bao la mapema la kiungo Amri Kiemba.
Hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na kiungo Amri Kiemba dakika ya pili.
Katika kubahatisha huko, Mbuyu Twite alifumua shuti zuri dakika ya 38 kutoka wingi ya kulia, ambalo lilitoka nje sentimita chache.
Katika dakika ya 63, beki Paul Ngalema aliunawa mpira katika harakati za kuokoa na refa Mathew Akrama akaamuru penalti, ambayo ilikwamisha kimiani kiufundi na Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Katika dakika ya 77 Mathew Amkrama alimtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Simon Msuva, baada ya kumkita Juma Nyosso, aliyemkanyaga ‘kwa bahati mbaya’. Msuva alichezewa rafu na Nyosso na tayari refa alikwishapuliza filimbi na kumpa kadi ya njano beki huyo wa Simba, lakini kiungo huyo wa Yanga akaponzwa na hasira za kitoto.
Pamoja na Yanga kubaki pungufu, waliendelea kucheza vema na mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili. Refa Akrama alishindwa kuumudu mchezo na maamuzi yake mengi yalikuwa chungu kwa Yanga, mfano Haruna Moshi ‘Boban’ alipomchezea rafu mbaya beki Kevin Yondan hadi akashindwa kuendelea na mchezo, na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Abdul alimpoza kwa kadi ya njano.
Hakumchukulia hatua yoyote kipa Juma Kaseja aliyeonekana kupoteza muda tangu mwanzo, na alimpa onyo tu zaidi ya mara tatu.
Alipingia Abdul alikwenda kucheza beki ya kulia na Mbuyu Twite akahamia katikati kucheza na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 13, ndani ya mechi tano na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, wakati Yanga imefikisha pointi nane na kubaki nafasi ya tano, kwani Coastal Union imetoa sare ya 2-2 na JKT Oljoro mjini Arusha na kufikisha pointi tisa.
Matokeo haya yameifanya Simba iwe na Pointi 13 kwa Mechi 5 na Yanga kuwa na Pointi 8 kwa idadi hiyo hiyo ya Mechi.
VIKOSI:
SIMBA: Juma Kaseja,
Nassor Chollo, Paul Ngalema, Juma Nyosso, Shomary Kapombe, Amri Kiemba,
Edward Christopher, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Mrisho
Ngassa.
Akiba: Wilbert Mweta, Komabil Keta,
Paschal Ochieng, Kiggi Makassy, Salum Kinje, Daniel Akuffo, Abdallah
Juma na Ramadhan Chombo ‘Redondo’
YANGA: Yaw Berko, Mbuyu
Twite, Oscar Joshua, Nadir Cannavaro, Kevin Yondan, Athumani Iddi,
Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi na
Hamisi Kiiza.
Akiba: Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma
Abdul, Godfrey Taita, Stafano Mwasyika, Job Ibrahim, Frank Domayo, Nizar
Khalfan, Shamte Ally, Idrisa Rajab na Jerry Tegete.
Refa: Mathew Akrama
No comments:
Post a Comment