Tuesday, November 7, 2023

KOCHA ROBERTO OLIVEIRA AFUKUZWA SIMBA, NI BAADA YA KIPIGO CHA BAO 5-1 KUTOKA KWA YANGA!!!

Klabu ya Simba SC imetangaza kuachana na Kocha wake Mbrazil, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo 'Robertinho' (63) baada ya miezi 10 tu kazini tangu alipowasili Januari 13, mwaka huu akitokea klabu ya Vipers ya Uganda.Taarifa ya Simba SC mchana huu imesema kwamba pamoja na Robertinho, pia kocha wa Fiziki, Mnyarwanda Cornoille Hategekimana naye ameondolewa na kwamba hivi sasa kitakuwa chini ya Mspaniola, Daniel Cadena aliyekuwa kocha wa makipa ambaye atafanya kazi pamoja na kocha wa timu za vijana, Suleiman Matola.
Simba SC imeachana na kocha mkuu Roberto Oliveira kufuatia kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa wapinzani wao Young Africans (Yanga SC) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Jumapili. Wekundu hao wa Msimbazi wamethibitisha katika taarifa yao kuwa wamefikia makubaliano ya kuachana na kocha huyo wa zamani wa Vipers SC sambamba na mkufunzi Corneille Hategemikana mara moja.

"Uongozi wa Simba unapenda kuwashukuru Oliveira na Hategemikana kwa mchango wao kwa timu wakati wa kukaa kwao na kuwatakia kila la kheri katika majukumu yao yajayo." Taarifa hiyo iliendelea kusema: “Tunapoendelea kutafuta kocha mpya, sasa timu itakuwa chini ya kocha Daniel Cardena akisaidiwa na Seleman Matola. Simba ilipata kipigo kizito zaidi dhidi ya wapinzani wao Timu ya Mwananchi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

No comments:

Post a Comment