
Hii ni Mechi ya pili mfululizo Simba kutoka sare kufuatia ile ya 0-0 hivi juzi huko Mkwakwani, Tanga na Coastal Union.
Bao za Simba zilifungwa na Felix Sunzu na Mrisho Ngassa na zile za Kagera kufungwa na Themi Felix na Salum Kanoni kwa Penati.
Kwenye mechi nyingine zilizochezwa leo,
Azam FC, ambao wako nafasi ya pili, walitoka sare 0-0 huko Mbeya na
Prisons na Mgambo KT, Timu iliyoanza Ligi kwa kudorora, leo imeshinda
Mechi yake ya 3 mfululizo kwa kuitandika Toto africans bao 2-0 huko
Mkwakwani Tanga.
Simba wakishangilia bao lao la kwanza katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar leo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka 2-2.

Beki wa Kagera, Amandus Nesta akiokoa mbele ya Sunzu

Nesta akimdhibiti Haruna Moshi wa Simba

Benjamin Effe akimdhibiti Mrisho Ngassa

Kipa wa Simba, Juma Kaseja akupangua mpira uliopigwa langoni mwake

Benjamin Effe akipiga shuti linalookolewa na Mwinyi Kazimoto

Kocha Mkuu wa Kagera, Abdallah Athumani Seif 'Kibadeni' kulia akiwa na Msaidizi wake, Mrage Kabange

Kikosi cha Kagera Sugar leo

Kikosi cha Simba leo

VIKOSI.
Kaseja, Chollo, Maftah, Nyoso, Ochieng, Kazimoto, Ngassa, Kiemba, Sunzu, Boban, Okwi.
Sub:
Mweta, Ngalema, Hassan Hatibu, Jonas Mkude, Uhuru, Kinje na Edward Christopher
MATOKEO:
Jumatano Oktoba 17
Tanzania Prisons 0 Azam 0
Polisi Morogoro 0 JKT Ruvu 2
Simba 2 Kagera Sugar 2
Mgambo JKT 2 Toto Africans 0
JKT Oljoro 0 African Lyon 0
MSIMAMO VPL:
1 Simba Mechi 8 Pointi 18
2 Azam FC Mechi 7 Pointi 17
3 JKT Oljoro Mechi 8 Pointi 13
4 Kagera Mechi 8 Pointi 12
5 Yanga SC Mechi 7 Pointi 11
6 Coastal Mechi 7 Pointi 10
7 JKT Ruvu Mechi 8 Pointi 10
8 Prisons Mechi 7 Pointi 9
9 Ruvu Shooting Mechi 7 Pointi 9
10 JKT Mgambo Mechi 8 Pointi 9
11 Mtibwa Sugar Mechi 6 Pointi 8
12 Toto African Mechi 8 Pointi 7
13 African Lyon Mechi 8 Pointi 7
14 Polisi Moro Mechi 8 Pointi 2
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Oktoba 20
Yanga v Ruvu Shootings
Coastal Union v Mtibwa Sugar [Mkwakwani, Tanga]
Jumapili Oktoba 21
JKT Ruvu v JKT Oljoro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mgambo JKT v Simba [Mkwakwani, Tanga]
Tanzania Prisons v Toto Africans [Sokoine, Mbeya]
No comments:
Post a Comment