BUKOBA SPORTS

Wednesday, October 17, 2012

WORLD CUP QUALIFIER: SPAIN 1 FRANCE1, GERMANY 4 SWEDEN 4 SWEDEN NJE!

>>GERMANY waongoza 4-0 na kutoka sare na Sweden 4-4!! >>MABINGWA SPAIN 1-1 na FRANCE!

Mechi ya Poland na England iliyokuwa ichezwe huko Warsaw  hapo jana ililazimika kuahirishwa kwa sababu ya mvua kubwa na Uwanja kujaa maji licha ya Uwanja huo wa kisasa kuwa na Paa ambalo huweza kufungwa na kufunguliwa lakini, katika hali ya utata, iliamuliwa lisifungwe kabla ya Mechi wakati utabiri ulikuwa ni wa Mvua kubwa.
Mechi hiyo imepangwa kufanyika leo.
Germany 4 Sweden 4
Germany wameivua ile rekodi yao ya ushindi kwa Asilimia Mia moja kwenye Kundi lao baada ya jana kuongoza kwa Bao 4-0 lakini Sweden wakapigana kiume na kulazimisha sare ya bao 4-4 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Olimpiki huko Munich, Germany.
Germany waliongoza kwa bao 2 ndani ya Robo Saa kwa bao za Moroslav Klose na Sentahafu Per Mertesacker kupiga bao la 3.
Katika Dakika ya 56, Mersut Ozil akafunga bao la 4 na kuifanya Germany iwe mbele kwa bao 4-0.
Ndipo katika Dakika ya 62, Sweden, wakiongozwa na Nahodha wao Zlatan Ibrahimovic, wakaanza kurudisha mabao kwa bao la kichwa la Ibrahimovic kufuatia pasi ndefu ya Kim Kallstrom.
Mikael Lustig akapiga bao moja na Johan Elmander akapiga bao la 3 na kuifanya ngoma iwe 4—3 katika Dakika ya 76.
Rasmus Elm akafunga bao la 4 na la kusawazisha Dakika za mwisho.
Germany bado wanaongoza Kundi C wakiwa na Pointi 10 kwa Mechi 4 wakifuatiwa na Sweden wenye Pointi 7 kwa Mechi 3.

Spain 1 France 1
Mchezaji wa France, ambae ni Straika wa Arsenal, Olivier Giroud, alitoka Benchi na kuifungia bao la kusawazisha katika dakika za mwisho na kuwafanya kutoka sare na Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Spain, ya bao 1-1 katika Mechi ya Kundi I iliyochezwa huko Madrid.
Sergio Ramos ndie aliefunga bao la Spain katika Dakika ya 25 na baadae Kipa wa France Hugo Lloris, anaedakia Tottenham, aliokoa Penati iliyopigwa na Cesc Fabregas.
Spain, ambao watarudiana na France Machi Mwakani huko Ufaransa, bado wanaongoza Kundi hili kwa ubora wa magoli wakiwa na Pointi 7 sawa na France kwa Mechi 3 kila mmoja.


MATOKEO:
Jumanne Oktoba 16
Russia 1 Azerbaijan 0
Israel 3 Luxembourg 0
Belarus 2 Georgia 0
Andorra 0 Estonia 1
Latvia 2 Liechtenstein 0
Bosnia-Hercegovina 3 Lithuania 0
Czech Republic 0 Bulgaria 0
Romania 1 Netherlands 4
Ukraine 0 Montenegro 1
Cyprus 1 Norway 3
Faroe Islands 1 Rep of Ireland 4
Croatia 2 Wales 0
Hungary 3 Turkey 1
Iceland 0 Switzerland 2
Macedonia 1 Serbia 0
San Marino 0 Moldova 2
Slovakia 0 Greece 1
Austria 4 Kazakhstan 0
Belgium 2 Scotland 0
Germany 4 Sweden 4
Italy 3 Denmark 1
Albania 1 Slovenia 0
Spain 1 France 1
Poland v England [IMEAHIRISHWA KUCHEZWA LEO]
Portugal 1 Northern Ireland 1
 
FAHAMU:
-ULAYA yapo Makundi 9
-Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.

No comments:

Post a Comment