Nigeria mabingwa wapya Afrika 2013,yailaza Burkina Faso 1-0 katika mchezo wa fainali nchini Afrika Kusini.
Ni shangwe na vigelegele katika miji mbalimbali nchini Nigeria baada ya timu yao ya The Super Eagles, kuibuka mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mbio za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika zilizoanza tarehe 19 Januari zimehitimishwa, Jumapili, tarehe 10 Februari kwa Nigeria kuibuka bingwa wa fainali za mwaka 2013 barani Afrika.
Bao la mchezaji Sunday Mba alilofunga katika dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza cha mchezo mjini Johannesburg, ndilo lililowahakikishia The Super Eagles, Nigeria kuwa mabingwa wapya.
Mchezo huo ulianza kwa kasi, timu zote mbili
zikishambuliana kwa zamu. Hata hivyo Nigeria ndiyo walionekana kutawala
zaidi mpambano huo na kukosa magoli kadha ambayo yangeipa ushindi mnono
Nigeria.
Vijana hao wa Super Eagles, wamekuwa wakiimarika kila hatua ya mashindano hayo, hasa baada ya kufuzu kutoka katika makundi. Ni katika hatua ya makundi ambapo mabingwa watetezi, Zambia walitolewa na kuachia kombe hilo kufukuziwa na timu nane zilizoingia robo fainali, na hatimaye timu mbili zilizotinga fainali, Nigeria na Burkina Faso.
Emmanuel Emenike aliibuka mfungaji bora wa
mashindano hayo na kupata kikombe, huku Moses Victor akiwa mchezaji bora
wa mechi kati ya Nigeria na Burkina Faso.
Mechi hiyo ya fainali ilihudhuriwa na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akiwa mgeni rasmi, akiambatana na rais wa Fifa Sepp Blatter na rais wa CAF, Issa Hayatou.
The Super Eagles pia waliahidiwa zawadi kem kem, zikiwemo fedha taslim kwa kocha na wachezaji, hata kabla ya kutwaa ubingwa.
Hii ni zawadi kubwa kwa kocha wa Super Eagles, Stephen Keshi ambaye mwaka 1994, wakati Nigeria ilipotwaa ubingwa wa Afrika, alikuwa nahodha wa timu hiyo katika fainali zilifanyika nchini Tunisia.
Pia Nigeria ilitwaa ubingwa mwaka 1980, wakati fainali hizo zilipoandaliwa nchini Nigeria.
Super Eagles kama ilivyo kwa timu nyingine barani Afrika, itakuwa ikijiandaa kikamilifu kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Mady Panandetiguiri na kipa Vincent Enyeama
Mchezaji wa Nigeria Victor Moses akichuana na Bakary Kone (katikati)Mba akifanya mambo yake
Kipa wa Burkina Faso Daouda Diakite akipangua mpira Mchezaji wa Nigeria Elderson Echiejileakiondolewa uwanjani baada ya kuumia
VIKOSI:
Ni shangwe na vigelegele katika miji mbalimbali nchini Nigeria baada ya timu yao ya The Super Eagles, kuibuka mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mbio za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika zilizoanza tarehe 19 Januari zimehitimishwa, Jumapili, tarehe 10 Februari kwa Nigeria kuibuka bingwa wa fainali za mwaka 2013 barani Afrika.
Bao la mchezaji Sunday Mba alilofunga katika dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza cha mchezo mjini Johannesburg, ndilo lililowahakikishia The Super Eagles, Nigeria kuwa mabingwa wapya.
Vijana hao wa Super Eagles, wamekuwa wakiimarika kila hatua ya mashindano hayo, hasa baada ya kufuzu kutoka katika makundi. Ni katika hatua ya makundi ambapo mabingwa watetezi, Zambia walitolewa na kuachia kombe hilo kufukuziwa na timu nane zilizoingia robo fainali, na hatimaye timu mbili zilizotinga fainali, Nigeria na Burkina Faso.
Mechi hiyo ya fainali ilihudhuriwa na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akiwa mgeni rasmi, akiambatana na rais wa Fifa Sepp Blatter na rais wa CAF, Issa Hayatou.
The Super Eagles pia waliahidiwa zawadi kem kem, zikiwemo fedha taslim kwa kocha na wachezaji, hata kabla ya kutwaa ubingwa.
Hii ni zawadi kubwa kwa kocha wa Super Eagles, Stephen Keshi ambaye mwaka 1994, wakati Nigeria ilipotwaa ubingwa wa Afrika, alikuwa nahodha wa timu hiyo katika fainali zilifanyika nchini Tunisia.
Pia Nigeria ilitwaa ubingwa mwaka 1980, wakati fainali hizo zilipoandaliwa nchini Nigeria.
Super Eagles kama ilivyo kwa timu nyingine barani Afrika, itakuwa ikijiandaa kikamilifu kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Mady Panandetiguiri na kipa Vincent Enyeama
Mchezaji wa Nigeria Victor Moses akichuana na Bakary Kone (katikati)Mba akifanya mambo yake
Kipa wa Burkina Faso Daouda Diakite akipangua mpira Mchezaji wa Nigeria Elderson Echiejileakiondolewa uwanjani baada ya kuumia
VIKOSI:
Nigeria: Enyeama, Echiejile (Oshaniwa, 64), Omeruo, Oboabona, Ambrose, Onanzi, Mikel, Mba (Yobo, 89) , Moses, Ideye, Uche (Musa, 54).
Yellow card: Onanzi, Oshinawa, Ideye
Scorer: Mba, 40
Burkina Faso: Diakite, Koffi, Kone, Koulibaly (Dagano), Panandetiguiri, Kone, Kabore, Rouamba (Sanou, 64), Nakoulma, Pitroipa, Bance.
Yellow card: Rouamba
Referee: Djamel Haimoudi (Algeria)

No comments:
Post a Comment