Mshambulizi wa Ivory Coast, Didier Drogba, ameshiriki katika mechi yake ya kwanza na klabu yake mpya ya Galatasaray na kuifungia bao moja na kuisadia kuilaza Akhisar ya Uturuki kwa magoli mawili kwa moja. Mchezaji huyo wa zamani Chelsea, alijumuishwa katika kikosi hicho kwa mchezaji wa akiba.
Drogba aliingia uwanjani kunako dakika ya sitini na tatu na dakika tano baadaye akaifungia Galatasaray bao lake la kwanza kwa kichwa.
Drogba amesaini mkataba wa miezi kumi na minanai nwa Klabu hiyo, baada ya kukihama klabu ya Shanghai Shenhua.
Hata hivyo klabu hiyo ya Uchina ilipinga uhamishwa huo wa Drogba, ikidai kuwa bado angali mchezaji wake kwa kuwa alikuwa amesaini mkataba wa miaka miwili.
Buruk Yilmaz naye akafaunga bao la pili na kuipa Galatasaray uongozi wa magoli mawili kwa bila.
Kufikia sasa galatasaray inaongoza kwenye msururu wa ligi kuu ya premier nchini Uturuki kwa zaidi ya alama nane.
Klabu hiyo imepangiwa kuchuana na Schalke 04 ya ujerumani siku ya Jumatano katika raundi ya tatu ya michuano wa kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Drogba aliiongoza Chelsea kushinda kombe hilo msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment