Wachezaji wa Swansea wakisherehekea ushindi wa Capital One Cup baada ya kuibamiza Bradford bao 5-0
Captain Ashley Williams na wachezaji wenzake wakishangilia ushindi huo mnono na wa historia baada ya miaka mingi kupita na kubeba kombe hilo kwa hamu kubwa. Hadi mapumziko, Swansea walikuwa mbele kwa Bao 2-0 kwa Bao za Nathan Dyer na Michu na Kipindi cha Pili kilipoanza tu, Dyer akapiga Bao la 3 na hilo likiwa Bao lake la pili.
Katika Dakika ya 91, Guzman alipachika Bao la 5 kwa Swansea na kuifanya Klabu yake ipate ushindi mkubwa kabisa katika historia ya Ligi Cup na kuupiku ule wa 4-0 Manchester United ilipoitwanga Wigan Mwaka 1996. Kwa kutwaa CAPITAL ONE CUP, Swansea City watacheza EUROPA LIGI Msimu ujao.
Swansea City na kombe lao la Capital One Cup wakishangilia kwa furaha na kiu ya muda mrefu kupita bila mafanikio na hatimaye kuliapata kwa mwaka huu wa 2013.
Wachezaji wa Bradford Citywakionekana hoi..baada ya kufungwa mvua ya magoli bila hata la kufutia machozi.
Nathan Dyer ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipatia goli la kwanza Swansea dakika ya 16.
Dyerakishangilia baada ya kuziona nyavu za Bradford.
Live Dyer na Williams mbele ya meneja Laudrup wakipeta!!..pamoja na Swansea kushinda pia walikosa nafasi nyingi za kufunga Bradford.
Michu nae hakusita kuipatia bao Swansea City kama kawaida yake na hapa akiipatia goli la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Bradford. Michu alipitisha shuti lake pembeni ya beki na pia kumpita kipa wa Swansea City upande wa pili.
Michu akijionea mpira huo ukiingia ndani ya goli la Bradford.
Michu akishangilia bao lake
Baada ya kazi nzuri na hapa ni wachezaji wa Swansea City wakielekea mapumzikoni na wakiwa mbele kwa bao 2-0 dhidi ya Bradford City.
Dyer akitupia dakika chache baada ya kuingia kwa ungwe ya kipindi cha pili na kufanya goli kuwa 3-0
Hakuna ... Dyer akiimaliza Bradford ambao walikuwa mwiba kwa mzee Wenger siku za nyuma kidogo.
Kipa wa Bradford City Matt Duke akimtega na kuanguka chini eneo la penati mchezaji wa Swansea Jonathan de Guzman na refalii kudai mpira utengwe penati.
Duke akioneshwa kadi nyekundu na refalii Kevin Friend
Kasheshe...De Guzman na Dyer kila mmoja akililia kupiga hat-trick.. De Guzman anadai kuwa yeye
ndiye kaangushwa lazima aipige yeye..muziki ...ishu ikaishia kwa aliye na mpira!!
De Guzman akafanikiwa kuipata hiyo penati na kuondoa gundu..
Ndani ya nyavu...
De Guzmanakuishia hapo aliongeza goli jingine dakika za lala salama.
Bw. Phil Parkinson akijionea mashabiki wa Bradford City wakiendelea kuishangilia timu yao japo kuwa wameishafungwa magoli mengi ambayo hata kurudisha matumaini haiwezekani...
Hakunaga!!!
Kidume.. Dyer akinyanyua juu kombe na zawadi yake uwanjani Wembley
Hoi....hoi....kwisha!
Kapteni wa Bradford City c Jones akiwashukuru mashabiki kwa sapoti zao mpaka mwisho!!
Ushindi mtamu... meneja wa Swansea Laudrupakibebwa juu juu ..
Wachezaji wa Swansea Citywakishangilia kwa aina yao ushindi huo wa Capital one cup uwanjani Wembley
VIKOSI:
Bradford: Duke, Darby, McHugh, McArdle, Good (Davies 46), Atkinson, Jones, Doyle, Thompson (Hines 73), Wells (McLaughlin 57), Hanson.
Subs Not Used: Ravenhill, Reid, Connell, Turgott.
Sent Off: Duke (56).
Swansea: Tremmel, Rangel, Williams, Ki (Monk 62), Davies (Tiendalli 84), Dyer (Lamah 77), Britton, de Guzman, Routledge, Hernandez, Michu.
Subs Not Used: Vorm, Shechter, Moore, Agustien.
Booked: Ki.
Goals: Dyer 16, Michu 40, Dyer 47, de Guzman 59 pen, 90.
Att: 82,597
Ref: Kevin Friend
Subs Not Used: Ravenhill, Reid, Connell, Turgott.
Sent Off: Duke (56).
Swansea: Tremmel, Rangel, Williams, Ki (Monk 62), Davies (Tiendalli 84), Dyer (Lamah 77), Britton, de Guzman, Routledge, Hernandez, Michu.
Subs Not Used: Vorm, Shechter, Moore, Agustien.
Booked: Ki.
Goals: Dyer 16, Michu 40, Dyer 47, de Guzman 59 pen, 90.
Att: 82,597
Ref: Kevin Friend
No comments:
Post a Comment