BUKOBA SPORTS

Monday, February 18, 2013

FA CUP: MANCHESTER UNITED 2 vs READING 1

Manchester United wakiwa kwao Old Trafford usiku huu wameibuka na ushindi wa goli  2-1 dhidi ya Reading. Kipindi cha kwanza kilimalizika bila timu yoyote kuziona nyavu za mwenzake licha ya kuumia kwa mchezaji wa United Jones na kulazimika kutolewa nje na nafasi yake kuingia Luis Nani dakika ya 42 kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana na kwa kasi zaidi, Dakika ya 69 Luis Nani akitokea benchi akaipatia goli la kwanza Manchester united kwa shuti kali na dakika ya 72 Hernandez akaiongezea goli na kufanya 2-0 dhididi ya timu ya Reading.
Dakika ya 81 mchezaji wa Reading Jobi McAnuff akaipatia Reading goli baada ya mabeki wa United kufanya makosa na hatimaye Jobi kumalizia mpira huo nyavuni.
FA Cup quarter-final draw Oldham Athletic or Everton v Wigan Athletic Millwall v Blackburn Rovers Manchester City v Barnsley Manchester United or Reading v Middlesbrough or Chelsea The ties will take place on the weekend of the 9 and 10 March. 
Nani akishangilia baada ya kupachika bao la kwanza

Javier Hernandez akitupia kwa kichwa goli la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Reading usiku huu.
Nani akiwamaliza kwa shuti kali Reading ambao walikuwa wameweka ngumu kipindi cha kwanza

Hakunaga... Nani akishangilia

Sir Alex Ferguson akifurahia ushindi huo
Phil Jones chini akijinyoosha baada ya kuumizwa mguu na mchezaji wa Reading
Phil Jones akuweza kuendelea, nafasi yake ilichukuliwa na Luis Nani dakika 42 kipindi cha Kwanza.
VIKOSI:
Manchester Utd:De Gea, Smalling, Jones (Nani 42), Vidic, Buttner, Valencia, Anderson (Carrick 83), Cleverley, Young (Van Persie 63), Welbeck, Hernandez.
Subs not used: Lindegaard, Ferdinand, Giggs, Kagawa.
Goals: Nani 69, Hernandez 72.
Reading: Federici, Kelly, Shorey, Mariappa, Morrison, Karacan, Leigertwood (Guthrie 63), McAnuff, McCleary (Robson-Kanu 70), Hunt, Le Fondre.
Subs not used: Andersen, Gunter, Pearce, Carrico, Pogrebnyak.
Booked: Hunt.
Goal: McAnuff 81.
Ref: Andre Marriner.

No comments:

Post a Comment