Kocha mkuu wa klabu ya Sion ya Uswisi Victor Munoz ameshushwa cheo na nafasi yake kuchukuliwa na Genaro Gatuso baada ya kipigo cha mabao 4-0 ilichokipata Sion kutoka kwa klabu ya Thun katika kombe la Uswisi maarufu kama Swiss super cup na badala yake amepewa majukumu mengine ya kutafuta vipaji vya wachezaji wa klabu hiyo.
Katika Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kwa vyombo vya habari imesema kwamba mpaka itakapoamuliwa vinginevyo, wachezaji wote wataendesha mambo yao wenyewe.Uongozi wa klabu umekabidhi majukumu yote kwa kapteni wa klabu hiyo Genaro Gattuso.
Klabu ya Sion inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya nchini Uswisi na ipo nyuma kwa alama tisa kwa vinara wa ligi hiyo timu ya Grasshoppers.
Gattuso ataanza kuitumikia klabu hiyo rasmi kama kocha katika robo fainali ya kombe la uswisi dhidi ya Lausanne.
Genaro Gattuso mwenye umri wa miaka 35 sasa na ambaye ni mchezaji wa nafasi ya kiungo wa zamani wa klabu ya Ac milan ya italia na Rangers ya Scotland anakuwa Kocha wa Tano wa klabu ya Sion kwa msimu huu akitanguliwa na kocha aliyeshushwa cheo mhispania Victor Munoz ambaye alianza kukinoa kikosi hicho mwezi januari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment