Manchester United walianza wao kufunga kupitia kwa mchezaji wao Danny Welbeck dakika ya 20 baada ya kupigwa kona na hatimaye kujitwisha mpira huo hadi nyavuni kwa kumpita Kipa wa Real Madrid upande wa pili.
Nalo goli la kusawazisha kwa timu ya Real Madrid lilifungwa na CR7 dakika ya 29 kwa kichwa baada ya kupigwa faulu na hatimaye Cristiano Ronaldo kuruka juu na kuuelekezea golini mwa United. Marudiano ni tarehe 5 mwezi wa tatu ndani ya Old Trafford.
Kipindi cha pili kilianza kwa Manchester United kushambulia lango la Real Madrid, hata hivyo mashambulio yaliigeukia Manchester United, huku mlinda mlango wake David de Gea akiokoa michomo mingi kutoka kwa vijana wa Real Madrid.
Alipoulizwa Mourinho kuhusu mpambano huo, anasema vijana wake walitawala mchezo huo, huku wapinzani wao wakisubiri kufanya mashambuliuo ya kushtukiza. Na kwa upande wa kumiliki mpira, Mourinho alisema timu zote zilicheza asilimia 50 kwa 50.
Hata hivyo kwa mujibu wa takwimu za mchezo huo, Real Madrid ilitawala kwa asilimia 54 dhidi ya 46.
VIKOSI:
Real Madrid:
Diego Lopez, Arbeloa, Sergio Ramos, Varane, Fabio Coentrao, Khedira,
Alonso (Pepe 83), Di Maria (Modric 75), Ozil, Ronaldo, Benzema (Higuain
60). Subs Not Used: Adan, Kaka, Carvalho, Essien. Goals: Ronaldo 30.
Man United: De Gea, Rafael, Ferdinand, Evans, Evra, Welbeck (Valencia 73), Carrick, Jones, Kagawa (Giggs 64), Rooney (Anderson 84), Van Persie.
Subs Not Used: Lindegaard, Smalling, Hernandez, Cleverley.
Booked: van Persie, Rafael, Valencia.
Goals: Welbeck 20.
Attendance: 85,454
Referee: Felix Brych
Man United: De Gea, Rafael, Ferdinand, Evans, Evra, Welbeck (Valencia 73), Carrick, Jones, Kagawa (Giggs 64), Rooney (Anderson 84), Van Persie.
Subs Not Used: Lindegaard, Smalling, Hernandez, Cleverley.
Booked: van Persie, Rafael, Valencia.
Goals: Welbeck 20.
Attendance: 85,454
Referee: Felix Brych
RATIBA/MATOKEO
Jumanne 12 Februari 2013
Celtic 0 Juventus 3
Valencia 1 Paris St Germain 2
Jumatano 13 Februari 2013
Real Madrid 1 Manchester United 1
Shakhtar Donetsk 2 Borussia Dortmund 2
Jumanne 19 Februari 2013
Arsenal v Bayern Munich
FC Porto v Malaga
Jumatano 20 Februari 2013
Galatasaray v FC Schalke
AC Milan v Barcelona
MARUDIANO
Jumanne 5 Machi 2013
Borussia Dortmund v Shakhtar Donetsk
Man United v Real Madrid
Jumatano 6 Machi 2013
Juventus v Celtic
Paris St Germain v Valencia
Jumanne 12 Machi 2013
Barcelona v AC Milan
Schalke v Galatasaray
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal
Malaga v FC Porto
No comments:
Post a Comment