TIMU ya wagosi wa kaya kutoka Tanga leo waliendeleza uteja kwa timu za mkoa huo baada ya ndugu zao JKT Mgambo kufungwa goli moja kwa sifuri na Kagera Sugar wiki iliyopita kwenye uwanja huu huu wa Kaitaba mjini Bukoba.
Dakika ya 58 kipindi cha pili mchezaji Felix Temi aliyetokea bench aliipatia goli la kuongoza timu yake kwa njia ya kichwa baada ya mabeki wa Coastal Union kujisahau na golikipa Shaaban Kado kuwategemea wao matokeo yake ikawa aibu kwa wagosi.
Mpira wa leo uliandamwa na mazengwe ya kila namna hata kufikia refa kutoa kadi mbili nyekundu moja kwa kila timu.
Kadi ya kwanza ilikuwa ni njano mbili ambazo alipewa mfungaji pekee wa mchezo wa leo Felix Temi baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu waku kujibishana na mwamuzi baada ya kukaa mbele ya mpiga mpira wa adhabu ndogo kinyume na taratibu.
Kadi ya pili ilipatikana dakika ya 71 baada ya mchezaji wa Kagera Sugar Laban Kambole kumsukuma Gabriel Barbosa, lakini Barbosa alipoamua kujibu mashambulizi kwa kumsukuma mpaka kuanguka chini, mwamuzi wa pembeni alimwashiria mwamuzi wa kati ampe kadi nyekundu.
Kitu hicho kiliamsha jazba uwanjani hasa ikizingatiwa Kagera Sugar walikuwa mbele kwa goli moja hivyo ilionekana ni hujuma dhidi ya Costal Union.
Mechi nyingine zilizochezwa leo na matokeo yake ni: Yanga 4-0 African Lyon, Mgambo JKT 2- 0 JKT Oljoro, Mtibwa Sugar 0-0 Ruvu Shooting, Toto Africa 2-2 Polisi Morogoro.
Wadau mbalimbali
No comments:
Post a Comment