Mashindano ya ligi daraja la tatu Mkoa wa Kagera yamefikia tamati hii leo Muleba Timu ya Biharamulo ikichinja timu ya Eleven Stars ya Misenyi Mtukula kwa jumla ya mabao 2-1. Biharamulo imehitimisha wiki ya furaha baada ya kunyakua ubingwa wa Kombe la Mkoa wa Kagera, Ligi iliyoshirikisha timu kadhaa za hapa Kagera na kufanyikia kwenye Uwanja wa Muleba.
Katika mchezo wa leo, Timu ya Biharamulo ilimenyana kiume na Eleven Star ya Mtukula ambayo ilionekana kuinuka vizuri katika safu yake na hasa baada ya kuifunga timu ya Kashai FC bao 3-0 juzi. Timu ya Eleven Stars katika mpambano wa leo ndiyo iliyoanza kupata bao kupitia mchezaji wao hatari Pascal na kisha Biharamulo kusawazisha kuwa 1-1. Bao la pili likafungwa na kapteini wao Hashim Idrisa baada ya kumchambua kipa wa Eleven na kuutokomeza mpira nyavuni. Timu ya Eleven Stars ikiwa ya pili ikifuatia na Kivuye FC na wa nne ni Kashai FC.
Wachezaji wa Biharamulo wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe lao.
No comments:
Post a Comment