Mabango yaliyobebwa na mashabiki waliofika uwanja wa ndege yakiwa na ujumbe mbalimbali
Rage akiwapungia mashabiki waliokuja kumlaki uwanja wa ndege
Mtu aliyevaa shati jeupe akipewa kichapo na mashabiki waliokuwepo uwanja wa ndege
Mashabiki wakisukuma gari la Rage baada ya kutokea gate la VIP
MWENYEKITI wa Simba Alhaj Aden Rage amerejea nchini akitokea India na kupokelewa kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali yaliyokuwa yamebebwa na mashabiki wa timu hyo yenye makazi yake mitaa ya Msimbazi Kariakoo.
Ragw ambaye alitua majira ya saa 10.30 jioni na kushukia VIP alikuwa anasubiriwa na mashabiki wanaomuunga mkono huku wale ambao hawamkubali wakivurumishwa eneo hilo mara baada ya kufika.
eneo
Vijana hao wachache waliofika eneo wakiwa wamekunja mabango yao wakati wanaomuun ga mkono rage walifika wakiwa wameyaweka hadharani na kusomeka kwa kila mtu walikimbizwa hadi wakatolewa nje ya eneo la uwanja wa ndege
Baada ya kuwasili eneo hilo Rage aliwasalimia mashabiki hao na kuondoka nao hadi Kariakoo yalipo makao makuu ya Simba na kwenda kuwahutubia.
Awali akiwa uwanja wa ndege waandishi wa habari walimuuliza anasemaje kuhusu mapinduzi yaliyo na wanachama na yeye alisema hajui kama Simba kuna mapinduzi na kama yapo mbona amekuja kupokelewa na mashabiki.
Msafara wa mashabiki uliongozwa na Makamu Mwenyekiti mzee Kinesi na Afisa Habari Ezekiel Kamwaga na viongozo wengine
No comments:
Post a Comment