Sunday, May 5, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: LIVERPOOL 0 v EVERTON 0, MAJOGOO WAKAMATIKA KWA EVERTON.


Leo kwenye mchezo wa Mahasimu majogoo Liverpool na Everton, Everton wakiwa ugenini kwenye eneo la Merseyside wameshindwa kutumia nafasi za wazi kwa kila timu na hatimaye kutoka kwa sare ya bila kufungana. Sare hii ikiwaweka katika nafasi Everton ya kushika nafasi ya 6 kwenye msimamo wakiwa na alama 60 juu ya majogoo Liverpool wenye alama 55 juu ya West Brom.

Kila upande ulikosa nafasi kwa Marouane Fellaini kuikosesha Everton kwa kupiga nje na Daniel Sturridge alipata nafasi safi kwa Liverpool lakini Kipa Tim Howard akaokoa.
Beki wa Everton Sylvain Distin alifunga Bao kwa kichwa lakini Refa akakataa Bao hio kwa madai Jamie Carragher, Mchezaji aliekuwa akicheza Dabi yake ya mwisho kwa vile anastaafu mwisho wa Msimu huu, alichezewa rafu.
Kocha wa Everton David Moyes na Liverpool kocha wa Liverpool Brendan Rodgers wakiangalia mtanange mchana huuMashabiki wa Everton wakiwasha moto uwanjani hapo kuwapa sapoti ya nguvu

Steven Pienaar akijaribu kuachia shuti kali ili kuipatia bao EvertonLucas na Leon Osman wakienda sawa leo mchana wakati wa mtanange wao kihasimuJamie Carragher wa Liverpool akimlaumu kocha Michael Oliver kuhusu mpambano wao na Everton Baada ya hatua hiyo shabiki wa Liverpool alionekana kunyanyua jezi ya Jamie Carragher juu.Philippe Coutinho akianguka chini kujiuguza baada ya mchezaji wa Liverpool Leon Osman kumfanyia ndivyo sivyo.Patashika hapa...Everton chupu chupu waifunge Liverpoolkumbuka mechi hii ni moja wapo ya kifungo cha mechi 10 za Luis Suarez alizofungiwa, Na leo hii ameutazamia mpira huu nje kama shabiki wa kawaida.
RATIBA/ MATOKEO
[Saa 9:00 Mchana]

Liverpool 0 v Everton 0
[Saa 12 Jioni]
Man United v Chelsea

Jumatatu Mei 6
[Saa 4:00 Usiku]

Sunderland v Stoke
Jumanne Mei 7
[Saa 3:45 Usiku]
Man City v West Brom
Wigan v Swansea
Jumatano Mei 8
[Saa 3:45 Usiku]
Chelsea v Tottenham
Jumamosi Mei 11
[Saa 8:45 Mchana]
Aston Villa v Chelsea

No comments:

Post a Comment