LIVERPOOL wametolewa jasho na Aston Villa, lakini wakapata pointi tatu walizozifuata huko ugenini Witton, Birmingham. Ilikuwa heka heka na mtafutano tangu kipindi cha kwanza.
Bao la dakika ya 21 kipindi cha Kwanza la Daniel Sturridge limewapa ushindi Liverpool wa alama tatu muhimu kwenye mchezo wa ligi kuu England leo wakicheza na Aton Villa ambao leo walikuwa wanacheza mchezo wao wa tatu, Aton Villa mechi ya kwanza walicheza na Gunners na kuwafunga bao 3-1, mechi yao ya pili walichjeza juzi na Chelsea na kufungwa bao 2-1 na leo hii wamenyukwa bao 1-0 bao la Daniel Sturridge. Villa leo wamecheza mchezo wa spidi kubwa na wakitaka kuifunga Liverpool lakini kukosa umakini ndiyo umewaangusha mpaka dakika ya 90 ya mchezo huo. Bao la pekee na la ushindi limepatikana dakika ya 21 kupitia kwa Daniel Sturridge baada ya kukatiza katikati ya mabeki wa Villa. Ushindi huu wa alama tatu muhimu unaweka pazuri Liverpool.Mchezaji Daniel Sturridge wa Liverpool akishangilia baada ya kuipachikia bao timu yake katika dakika ya 21 leo hii walipocheza ugenini na timu ya Aston Villa kwenye uwanja wao wenyewe Villa Park huko Birmingham, England.
Daniel Agger na kipa wa Villa Brad Guzan kwenye patashika!!!!Christian Benteke na Glen Johnson wakichuana vikali hapa..Gabriel Agbonlahor akikosa kosa mpira kuuvuta hapa dhidi ya Steven Gerrard
Kolo Toure na Christian Bentekekwenye majanga eneo la penati...
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Lowton (EL Ahmadi 65), Vlaar, Okore, Luna, Bacuna, Westwood, Delph, Weimann (Tonev 73), Benteke, Agbonlahor.
Subs: Clark, Helenius, Steer, Herd, Sylla.
Booked: Luna, Delph, Lowton.
Liverpool: Mignolet, Johnson, Toure, Agger, Jose Enrique, Gerrard, Lucas, Henderson, Aspas (Cissokho 69), Coutinho, Sturridge.
Subs: Brad Jones, Alberto, Allen, Borini, Sterling, Wisdom.
Goal: Sturridge 21.
Booked: Aspas.
Referee: Mark Clattenburg (Tyne & Wear)
No comments:
Post a Comment