Kigogo hicho cha Hispania bado kipo katika mazungumzo juu ya ada ya uhamisho wake mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 uhamisho unatarajiwa kuwa ni wa pauni milioni £86.
Spurs kutoka London ya kaskazini imekuwa katika harakati za kusajili wachezaji wa kimataifa sita wakitumia zaidi ya pauni milioni £90.
Hii leo klabu hiyo imethibtisha kumsajili mshambuliaji wa Roma, Erik Lamela na mlinzi wa Steaua Bucharest Vlad Chiriches ikiwa ni nyongeza baada ya kuwasili kwa kiungo Etienne Capoue na Paulinho, winga Nacer Chadli na mshambuliaji Roberto Soldado.
Bado wanasaka saini ya ya mdenishi kiungo Christian Eriksen kutoka katika klabu ya Ajax
No comments:
Post a Comment