AC Milan walitangulia kwa Bao la Dakika ya 14 alilofunga Andrea Poli ambae alikuwa akiichezea Klabu yake mpya Mechi ya kwanza tu.
Lakini vichwa viwili vya Mkongwe Luca Toni, Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Italy, vya Dakika za 29 na 53 viliipa Hellas Verona ushindi wa Bao 2-1 katika Mechi yao ya kwanza ya Msimu mpya wa Ligi na pia ikiwa ni mara yao ya kwanza kucheza Serie A katika Miaka 11.
Ushindi huo ulileta furaha kubwa na hoihoi kwa Mashabiki wa Hellas Verona waliojazana Stadio Bentigodi ambao kwa Miaka mingi waliteseka wakiona Timu yao ikigaagaa Madaraja ya chini ya Ligi yale ya Pili na ya Tatu wakati Mahasimu wao wakubwa wa Mji mmoja, Chievo Verona, wakimeremeta Ligi kubwa ya Serie A.
Balotelli jana hakuwa sawa alishindwa kufanya makeke kuipatia ushindi Millan na hatimaye kupata lawama kutoka kwa mashabiki...
Saturday, August 24, 2013
Sampdoria 0 Juventus 1 Bao hilo llifungwa katika Dakika ya 58 kufuatia kazi nzuri ya Arturo Vidal na Paul Pogba kwenye Kiungo.
Katika Dakika ya mwisho, Sampdoria walibaki Mtu 10 wakati Paolo Castellini, alieingizwa toka Benchi, kumchezea rafu mbaya Stephan Lichtsteiner na kupewa Kadi Nyekundu.
Serie A inaendelea tena leo kwa Mechi 7 na kesho Jumatatu Usiku iko Mechi moja.
SERIE A
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Agosti 24
Hellas Verona 2 AC Milan 1
Sampdoria 0 Juventus 1
Jumapili Agosti 25
19:00 Inter Milan v Genoa
21:45 SS Lazio v Udinese
21:45 Parma v Chievo Verona
21:45 Torino FC v Sassuolo
21:45 Napoli v Bologna
21:45 Livorno v AS Roma
21:45 Cagliari v Atalanta
Jumatatu Agosti 26
21:45 Fiorentina v Catania
No comments:
Post a Comment