Kenya itakuwa mwenyeji wa michuano ya Chalenji ya shirikisho la soka Afrika mashariki Cecafa.
Katibu mkuu wa Cecafa icholas Musonye amekaririwa hii leo akisema kuwa mamlaka ya soka nchini Kenya imethibtisha utayari wao wa kuandaa michuano hiyo.
Michuano hiyo ya kila mwaka ya ukanda wa nchi za Afrika mashariki imepangwa kuanza Novemba 24 na kumalizika Disemba 8.
Wakati wa baraza la Cecafa lilofanyika mjini Kampala nchini Uganda mwaka jana nchi za Rwanda na Kenya walionyesha nia ya kutaka kuandaa michuano hiyo.
Lakini hata hivyo chama cha soka cha Rwanda kimetaka chenyewe kuandaa mwakani ikiwa ni kipimo chao cha maandalizi ya kuandaa fainali ya michuano ya wachezaji wa ndani barani Afrika CHAN mwaka 2016.
Mara ya mwisho Kenya kuandaa ilikuwa ni mwaka 2009 ambapo Kenya ililalamikiwa kuwa na watazamaji wachache.
Musonye amezitaja nchi zinazo tarajiwa kushiriki kuwa ni pamoja na Tanzania bara, Zanzibar, Burundi, Eritrea, Somalia, Djibouti, Sudan, South Sudan, Burundi, Ethiopia, Rwanda, mabingwa watetezi Uganda na Kenya.
No comments:
Post a Comment