REFA Jonas Eriksson kutoka Sweden ametangazwa na UEFA kuwa ndiye Refa wa pambano
la UEFA Super Cup kati ya Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich na Washindi wa
EUROPA LIGI Chelsea litakalochezwa huko Stadion Eden Mjini Prague
Nchini Czech Republic hapo Ijumaa Agosti 30.
Eriksson, Miaka 39, amekuwa Refa wa Kimataifa tangu Mwaka 2002 na ameshachezesha Mechi 75 za UEFA.
Msimu uliopita, Eriksson alichezesha
Mechi 6 za UEFA CHAMPIONZ LIGI ikiwemo Robo Fainali kati ya Málaga CF na
Borussia Dortmund na pia kuchezesha Mechi 3 za EUROPA LIGI ikiwemo
Mechi ya pili ya Nusu Fainali kati ya Chelsea na FC Basel.
Kwenye Mechi hiyo ya UEFA Super Cup,
Eriksson atasaidiwa na wenzake kutoka Sweden Mathias Klasenius na Daniel
Wärnmark huku Stefan Wittberg akiwa Refa wa Akiba na Wasaidizi wa
Nyongeza ni Stefan Johannesson na Markus Strömbergsson.
UEFA SUPER CUP-WASHINDI WALIOPITA!
2012 Atlético
2011 Barcelona
2010 Atlético
2009 Barcelona
2008 Zenit
2007 Milan
2006 Sevilla
2005 Liverpool
2004 Valencia
2003 Milan
2002 Real Madrid
2001 Liverpool
2000 Galatasaray
1999 Lazio
1998 Chelsea
1997 Barcelona
1996 Juventus
1995 Ajax
1994 Milan
1993 Parma
1992 Barcelona
1991 Manchester United
1990 Milan
1989 Milan
1988 Mechelen
1987 Porto
1986 Steaua
1984 Juventus
1983 Aberdeen
1982 Aston Villa
1980 Valencia
1979 Nottm Forest
1978 Anderlecht
1977 Liverpool
1976 Anderlecht
1975 Dynamo Kyiv
1973 Ajax
No comments:
Post a Comment