Arsenal wako kileleni Pointi 2 mbele baada ya Jumamosi kushinda 2-1 Ugenini walipoichapa Swansea City na huo ni ushindi wao wa tano mfululizo toka kichapo cha Mechi ya kwanza kabisa walipofungwa 3-1 na Aston Villa.
Akiongea kabla Mechi yao ya Jumanne ya KUNDI F la UEFA CHAMPIONS LEAGUE, UCL, watakayochezea kwao Emirates na Napoli, Wenger alisema: “Tunataka uwiano mzuri kuhusu nia na unyenyekevu. Kuzungumzia Ubingwa leo hii ni upuuzi! ”
Wenger alisema walipofungwa na Villa kwenye Mechi ya kwanza yeye hakuwa na wasiwasi na kufafanua: “Watu wanasahau tulikuwa kwenye mbio ndefu za kutofungwa tangu Machi na ukichukulia hiyo kufungwa na Villa ni Mechi moja tu kati ya 21.
Moja ya sababu ya Arsenal kufanya vizuri ni fomu nzuri ya Kiungo wao Aaron Ramsey ambae ameshafunga jumla ya Bao 9 na 5 ni katika Gemu 4 za mwisho na pia Straika Olivier Giroud ambae mpaka sasa ameshafunga Bao 5.
No comments:
Post a Comment