Wakati Barca wanaichapa Real Sociedad
Bao 4-1 na kufikisha Pointi 18 kwa Mechi 6 na Atletico Madrid nao
wakaichapa Osasuna Bao 2-1 na kukamata Pointi 18 kwa Mechi 6.
Bao za Barca kwenye Mechi yao zilifungwa
na Neymar Dakika ya 5, Lionel Messi, ya 8, Sergio Busquets, ya 23 na
Marc Batra, ya 77 huku Bao la Real Sociedad likifungwa na lberto De La
Bella katika Dakika ya 64.
Bao za Atletico Madrid zote mbili zilifungwa na Costa na lile la Osasuna na Riera.
La Liga inaendelea tena leo Usiku kwa Real Madrid kucheza Ugenini na Elche pamoja na Mechi nyingine kadhaa.
Huko Germany Mechi za Raundi ya Pili ya
German DFB Pokal 2013/2014 zilinguruma na Borussia Dortmund walihitaji
Dakika 120 ili kuitoa TSV 1860 Munich baada kutoka 0-0 katika Dakika 90.
Bao za Borussia Dortmund zilifungwa na
Pierre‑Emerick Aubameyang kwa Penati ya Dakika ya 105 na Henrik
Mkhitaryan katika Dakika ya 107.
Mechi nyingine za German DFB Pokal
2013/2014 zinaendelea leo ambako Mabingwa Watetezi Bayern Munich
watacheza na Hannover pamoja na Mechi nyingine kadhaa.
Huko italy, kwenye Serie A, Jana
ilikuwepo Mechi moja tu ambayo Udnese iliifunga Genoa kwa Bao 1-0 na Bao
la ushindi kufungwa na Calaio katika Dakika ya 79 kwa kujifunga
mwenyewe.
Leo Usiku ziko Mechi lukuki za Serie A
ambapo pia Mabingwa Watetezi Juventus watakuwa Ugenini kucheza na Chievo
Verona na Vinara AS Roma wako Ugenini kucheza na Sampdoria huko Napoli,
waliofungana kwa Pointi na AS Roma, wako Nyumbani kucheza na Sassuolo.
SERIE A
Jumanne Septemba 24
Udinese 1 Genoa 0
Jumatano Septemba 25
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Bologna v AC Milan
Chievo v Juventus
Lazio v Catania
Livorno v Cagliari
Napoli v Sassuolo
Parma v Atalanta
Sampdoria v AS Roma
Torino v Hellas Verona
Alhamisi Septemba 26
Inter v Fiorentina
LA LIGA
RATIBA
Jumanne Septemba 24
Barcelona 4 v Real Sociedad 1
Levante 1v Valladolid 1
Atletico Madrid 2 v Osasuna 1
Malaga 2 v Almeria 0
Jumatano Septemba 25
2100 Granada v Valencia
2100 Sevilla v Rayo Vallecano
2300 Elche v Real Madrid
Alhamisi Septemba 26
2100 Athletic Bilbao v Betis
2300 Getafe v Celta Vigo
2300 Villarreal v Espanyol
No comments:
Post a Comment