BUKOBA SPORTS

Wednesday, September 25, 2013

CAPITAL ONE CUP: TOTTENHAM 4 v ASTON VILLA 0, SPURS WAFANYA KWELI!

MICHUANO ya kombe la mtoano la Capital One imefanyika jana usiku kwa Tottenham kuifunga Aston Villa 4-0 huku kukiwa na kituko cha aina yake pale mshambuliaji wa Aston Villa Nicklas Helenius alipojaribu kwenda kufunga licha ya kukabwa na beki Jan Vertonghen hadi bukta ikamvuka. Wakati Helenius anachanja mbuga kuelekea kwenye 18 ya Tottenham Vertonghen alihofia kuwa mshambuliaji huyu angeweza kusawazisha bao lao la kwanza lililofungwa na Defoe na hivyo akaamua kumdhibiti kwa kumvuta bukta. Nicklas Helenius akikosa mpira wakati  Aston Villa wakiumana na Spurs usiku wa kuamkia leo..
...Penati au...! Majanga!Jermain Defoe akiwapatia bao Spurs na kuongeza mashambulizi ...akishangilia hapa..baada ya kufunga bao Paulinho aliongeza la pili..!Nacer Chadli akawaua baada ya ktupia la tatu na kufanya 3-0 dhidi ya Aston Villa

No comments:

Post a Comment