BUKOBA SPORTS

Wednesday, September 11, 2013

FRIENDLY MATCH: BRAZIL 3 v PORTUGAL 1

 Mchezaji mpya wa Barcelona Neymar amekuwa Nyota wa Brazil walipoifunga Portugal Bao 3-1 katika Mechi ya Kirafiki iliyochezwa huko Gilette Stadium, Boston, Massachusetts Alfajiri ya Leo hii. 
Neymar alifunga Bao moja na kuwa na Mguu wake katika Bao nyingine mbili za Brazil.

Raul Meireles, ambae mapema alipiga kichwa kilichogonga posti, aliipa Portugal Bao la kuongoza katika Dakika ya 18 baada ya kutumia makosa makubwa ya Fulbeki Maicon alietaka kumrudishia kwa kichwa Kipa Julio Cesar na Mpira kunaswa na Meireles.
Lakini Neymar akawika na kupiga Kona iliyounganishwa kwa kichwa na Thiago Silva na kuwapa Bao la kusawazisha na kisha kufunga Bao la Pili lililowapa Brazil uongozi wa 2-1 hadi Mapumziko.

Dakika 4 baada ya Haftaimu, pasi murua ya Neymar ilimfungua Fulbeki Maxwell aliepiga krosi kwa Jo alietingisha nyavu na kuweka Bao la 3 kwa Brazil, hilo pia likiwa Bao lake la 3 baada ya Juzi kufunga Bao 2 wakati Brazil inaibomoa Australia 6-0 huko Brasilia.

Matokeo haya yamewafanya Brazil waendeleza Rekodi yao ya kutofungwa na Portugal katika Mechi 3 zilizopita ambapo wameshinda Mechi mbili za Kirafiki na kutoka 0-0 kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwaka 2010.
Mchezaji  Raul Meireles kushoto na Miguel Veloso kulia wakicheza kwa furaha na kwa kupongezana baada ya Raul kuipachikia bao Potugal mapeema dakika ya 18

Wachezaji wa  Portugal wakipongezana!

Bruno Alves na wenzake wakimweka mtu kati Neymar
Thiago Silva akipokea kwa kichwa mpira uliopigwa kwa kona na  Neymar na kuishiria nyavuni
Mchezaji Nani (kulia) akipagawa baada ya kukosa nafasi ya kufunga bao hapa! Neymar akiondolewa nje baada ya kufanya vizuri tangu kipindi cha kwanza na hapa akiwapa salaam kwa mbali mashabiki.
Mchezaji Jo akifunga bao la mwisho hapa
Joao Pereira kulia na  Paulinho kushoto kwenye patashika

VIKOSI:
Brazil: Julio Cesar, Maicon, Thiago Silva, Luiz, Maxwell, Paulinho (Henrique 83), Gustavo, Ramires (Oscar 61), Bernard (Hernanes 68), Jo (Pato 76), Neymar (Lucas Moura 89).  
Subs not used: Jefferson, Marcos Rocha, Fernando, Dante.
Booked: Neymar, Ramires.
Goals: Thiago Silva 24, Neymar 34, Jo 49
Portugal: Rui Patricio, Joao Pereira (Postiga 70), Pepe (Luis Neto 46), Bruno Alves, Fabio Coentrao (Antunes 54), Veloso, Vieirinha (Lica 84), Meireles, Joao Moutinho (Ruben Amorim 59), Nani, Nelson Oliveira.  
Subs not used: Eduardo, Andre Martins, Ricardo Costa, Adrien Silva, Josue, Lopes.
Booked: Pereira, Postiga, Bruno Alves.
Goal: Meireles 18.
Referee: Juan Guzman (USA).

No comments:

Post a Comment