BUKOBA SPORTS

Thursday, September 12, 2013

KOCHA WA CZECH MICHAL BILEK AJIUZULU.

KOCHA wa timu ya taifa wa Jamhuri ya Czech, Michal Bilek amejiuzulu wadhifa wake huo kufuatia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Italia kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia na kumaliza ndoto za nchi hiyo kushiriki michuano hiyo itakayofanyika nchini Brazil mwakani. Czech imekuwa ikisuasua katika kampeni zake za kufuzu chini ya Bilek wakiwa wamewafunga Malta na Armenia pekee katika mechi zao za kundi B.Katika taarifa yake Bilek amesema amefikia hatua hiyo ya kuachia ngazi kwasababu hawakufikia malengo waliyojiwekea. Bilek amekuwa akipigiwa kelele na mashabiki wa soka nchini humo wakihoji uwezo wake lakini kidogo alijenga uaminifu baada ya kuiwezesha Czech kufika robo fainali katika michuano ya euro 2012.

No comments:

Post a Comment