Wachezaji wakisalimi waamuzi muda mfupi kabla ya mtanange kuanza kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini.Wachezaji wa timu ya JKT Oljoro wakisalimiana na wenzao wenyeji Kagera Sugar.
Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya kagera Sugar imepata ushindi wa alama tatu muhimu kwenye ligi kuu Vodacom kwenye Uwanja wao wa Kaitaba leo hii, Kagera Sugar Ndiyo walianza kupata bao dakika ya 27 kipindi cha kwanza baada ya Mpira kurushwa kama kona na mpira huo kumaliziwa na mchezaji Godfrey Wambura. Kipindi hicho hicho cha kwanza Maafande JKT Oljoro wakasawazisha bao hilo kupitia mchezaji wao Shaibu Nayopa katika dakika ya 41. Bao la Ushindi likifungwa na timu Kapten Malegesi Mwangwa dakika ya 90 baada ya kupata kona nne mfululizo.
Timu kapteni wa pande zote mbili waliwasogelea waamuzi kujua timu zao zinaanza mtanage kuelekea pande ipi kwanza'
Kikosi cha timu ya Maafande kutoka Arusha JKT OljoroKikosi cha Kagera Sugar kilichoanza mtanange jioni hii kuumana na maafande JKT OljoroWaamuzi wa mtanange huo kati ya Kagera Sugar na JKT Oljoro
Benchi la timu ya JKT Oljoro (kushoto) ni kocha mkuu anayefata ni mganga(Docta) wa timu ya Oljoro
Benchi la timu ya JKT Oljoro (kushoto) ni kocha
Benchi la Kagera Sugar kulia ni kocha mkuu wa timu hiyo Jackson Mayanja na wanaofuata ni wasaidizi na Docta wa timu
Wachezaji wa akiba wa timu ya kagera sugar.
Mtanange ukiendelea!!
Dakika ya 27 mchezaji wa Kagera Sugar aliwapachikia bao la kwanza baada ya kurushwa mpira kama kona na kisha mchezaji Godfrey Wambura kumalizia mpira huo nyavuni.
Wachezaji wa Kagera sukari wakifurahia baada ya mchezaji wao Godfrey kuwapatia bao
Mechi hii ni ya pili kwa Kagera sugar kwenye uwanja wao wa Kaitaba baada ya jumamosi iliyopita kutoka sare na Azam Fc ya jijini Dar es salaam. Mchezo wa kumalizia kwenye uwanja huu kabla ya kuelekea mkoa mwingine (ugenini) Utakuwa ni Ashanti nayo ikitoka jijini Dar.
Dakika za lala salama kuanzia dakika ya 85 Timu ya Kagera Sugar iliandama bao la Maafande JKT Oljoro kwa kupata kona nyingi na dakika ya 90+1 wakapata bao kupitia kwa mchezaji Beki wa Timu hiyo Malegesi Mwangwa.
Angalia kona za mara kwa mara kwenye lango la JKT Oljoro wakati zikipigwa na lango lilivyokuwa linaonekama kwenye Taswira mbalimbali hapa.
Kona zilipigwa sana dakika za lala salama kuelekea lango la JKT Oljoro!! Na muda huo mashabiki wengi wakiwa wameisha kata tamaa na kuanza kuondoka kwenye uwanja wa Kaitaba na punde wakasikia bao na kurudi tena uwanjani!!
Mpaka Kagera Sugar wakapata bao dakika ya 90 kupitia kwa Malegesi Mwangwa!!
Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Malegesi katika dakika za majeruhi
Ilikuwa Patashika nguo kuchanika!! Kagera sugar wakipata ushindi dakika za lala salama!!!
Ongera Mwanetu!! Malegesi!! Ongera sana umetuokoa na Sare zetu ambazo hazina maana sana!!...
Furaha zikiwatanda wana Kagera Sugar hapa baada ya kuwashona bao la aina yake katika dakika za lala salama ...kama United Vile!!
Usipime!! ushindi Mtamu!!
No comments:
Post a Comment