Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson atazawadiwa ‘Uhuru wa Manispaa ya Trafford’ kwa kuiongoza Klabu hiyo kwa mafanikio makubwa. Ferguson aliiongoza Man United kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 13 na Ubingwa wa Ulaya mara 2 na kujisimika kama ndie Meneja mwenye mafanikio makubwa katika Historia ya Soka ya Uingereza. Gwiji huyo alimaliza utawala wake Man United uliodumu Miaka 26 hapo Mei na Manispaa ya Trafford huko Jijini Manchester imetamka kuwa atatunukiwa heshima ya ‘Uhuru wa Manispaa ya Trafford’ hapo Oktoba 14 kwenye Mkutano wa Madiwani wa Manispaa hiyo. Vile vile, Manispaa hiyo imeamua kubadili jina la Barabara iliyo karibu na Uwanja wa Old Trafford kutoka Walters Reach na kuuita Sir Alex Ferguson Way.
Akizungumzia kutunukiwa heshima hizo, Sir Alex Ferguson amesema: “Nina furaha kukubali heshima hii kutoka Manispaa ya Trafford. Nilipofika Old Trafford Mwaka 1986 sikujua safari inayoningoja mimi. Baada ya Robo Karne, kupewa ‘Uhuru wa Manispaa ya Trafford’ na sehemu ya Trafford kuitwa Jina langu ni heshima kubwa.” Nae Kiongozi wa Manispaa ya Trafford Matt Colledge amesema: “Sir Alex ametoa mchango mkubwa kwa Trafford kwa kipindi kirefu kwa uongozi wake shupavu wa Timu ya Manchester United na tumeona kumpa ‘Uhuru wa Manispaa ya Trafford’” na kuiita Mtaa Sir Alex Ferguson Way ni heshima anazostahili.” Aliongeza: “Soka inachangia sana maendeleo ya Manispaa yetu kwa kuvutia Wageni wengi na kutoa ajira nyingi. Ni kwa sababu ya mafanikio ya Timu ndio maana Klabu imeimarika na kuwa mojawapo ya Klabu zenye mafanikio makubwa na kujulikana sana Duniani.”
Sir Alex Ferguson aliacha kuiongoza mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuiongoza Uinted miaka 27.

Sanamu la Sir Alex Ferguson Old Trafford
No comments:
Post a Comment