Jengo la The Westgate Shopping Centre likianza kufuka moshi kufuatia shambulizi la kigaidi la Al Shabaabab kama linavyoonekana kwa mbali, ambapo watu wanaokadiriwa kufikia 69 wameripotiwa kuuawa. (Picha zote za tukio hilo juzi ni kwa Hisani ya Gazeti la Daily Mail la Uingereza)
Wanajeshi wakiwa katika ulinzi mkali wa kujaribu kukabiliana na waasi wa Al Shabaabab katika uvamizi huo huko Westgate.
Askari akitoa maelekezo ya njia za kukimbilia kwa baadhi ya waliobahatika kukimbia eneo hilo.
Vikosi vya usalama na uokoaji vikiwa katika harakati za kutoa misaada.
Polisi wa imeelezea uwepo wa mashambulizi baina ya vikosi vya usalama vya nchi hiyo na waasi hao.
Maofisa wa Polisi wa Kenya wakiwa katika doria eneo la tukio.
Wanajeshi wa Kenya huko Westgate Shopping Centre wakiwa katika mapambano na waasi.
Wanajeshi wakiwa kazini kupambana na waasi.
Watoto hawa wakiwa hawajui waende wapi wala wafanye nini, wamepigwa butwaa kutokana na hekaheka za tukio hilo.
Msamaria mwema akijiandaa kumchukua mtoto anayekimbia ovyo akiwa amepotezana na wazazi wake katika tukio hilo.
Mchoro kuonesha uvamizi ulivyofanyika.
Wanamama wakiwa amejibanza na watoto wao kujaribu kujiokoa.
Vikosi vya Jeshi la Kenya vikielekea katika kutoa msaada wa kiuokozi Westgate Shopping Centre jijini Nairobi.
Ndugu na jamaa wa majeruhi wakiwa katika foleni ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya ndugu zao.
No comments:
Post a Comment