
Wachezaji pande zote mbili wakisalimiana

Wachezaji wa Kagera Sugar wakiwasalimia wenzao Ashanti United kutoka jijini Dar es Salaam

Salaam zikiendelea uwanjani kabla ya mechi kuanza.

Waamuzi wa mtanange huu wakipata picha ya pamoja hapa.

Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza kumenyana na Ashanti United

Kikosi cha kilichoanza cha Kagera Sugar

Kikosi cha Ashanti United kilichoanza

Waamuzi na timu kapteni pande zote mbili wakiteta kuhusu mtanange huu na kujua uelekeo wa kila timu

Benchi la Ashanti United na viongozi wake

Benchi la Kagera Sugar kulia ni Kocha wake Uganda Jacksony Mayanja akiteta na kiongozi msaidizi Mlage Kabange kuhusu matanange huu

Mtanange ukiendelea.
Na Faustine Ruta, Bukoba
Bao la kwanza la kagera Sugar limefungwa na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Daudi Jumanne "Dunga" dakika ya 31 baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa Suleiman Kibuta.
Dakika ya 68 kipindi cha pili mchezaji aliyekuwa amekosakosa mabao kadhaa Suleiman Kibuta akaipachikia bao la pili baada ya kupita katikati ya mabeki wa timu ya Ashanti United na kutupia nyavuni. Temi Felix akamalizia bao la mwisho dakika ya 89 na kufanya 3-0 dhidi ya timu ya Ashanti United kutoka jijini Dar es salaam.
Kipa wa Ashanti akijionea mwenye timu yao kuzidiwa

Mashabiki

Kocha wa Kagera Sugar akisisitiza jambo uwanjani kuhusu kuziba nafasi zilizokuwa zimeachwa wazi na baadhi ya wachezaji wake.,

Kipa wa Ashanti United akidaka shuti kali kipindi cha pili lililopigwa na Temi Felix

Suleiman Kibuta akishangilia baada ya kufunga bao la pili dakika ya 68 kipindi cha pili.

Wachezaji wa Ashanti Unite kwenye mtanange huu hawakuwa makini sana kwani walicheza mchozo wa rafu sana na baadhi ya wachezaji kuambulia kupewa kadi za njano na kuwaletea tatizo uwanjani wakiepuka kupewa kadi ya pili na hatimaye kutolewa nje.

Furaha kwa mchezaji aliye funga bao la pili na hapa akipongezwa

Hongera sana!!!

Wachezaji wa Kagera Sugar wakipongezana jioni hii baada ya kuifunga bao la tatu na la mwisho kwenye dakika za majeruhi dakika ya 89 kipindi cha pili.
No comments:
Post a Comment