MWISHO wa wiki hii wachezaji wengi waliosajili kwenye dakika za mwisho za dirisha la usajili la majira ya Kiangazi walipata nafasi ya kucheza mechi zao za kwanza. Bingwa linaangalia kilichofanywa na wachezaji hao kwenye Ligi Kuu England ‘wikiendi’ hii.
Mesut
Ozil (Arsenal)
Thamani:
Pauni milioni 42.5 (sh bilioni 106.265)
Dakika
uwanjani: 80
Matokeo:
Arsenal 3-1 Sunderland
Maksi:
9/10
Alichofanya
Kama ilivyotarajiwa na wengi alifanya vizuri. Kiungo
huyo mchezeshaji alitengeneza bao moja na kuhakikisha kwamba Arsenal hawalioni
pengo la majeruhi Santi Cazorla na alimtengenezea Theo Walcott nafasi mbili za
wazi, lakini Muingereza huyo alishindwa kufunga. Ozil alitolewa uwanjani zikiwa
zimesalia dakika 10 mpira kwisha, mashabiki wote walisimama na kumpigia makofi,
Ozil anatabiriwa kuwa moto zaidi msimu ujao.
MAROUANE FELLAINI
Marouane
Fellaini (Manchester United)
Thamani:
Pauni milioni 27.5 (Sh bilioni 68.759)
Dakika
uwanjani: 28
Matokeo:
Man United 2-0 Crystal Palace
Maksi:
6/10
Alichofanya
Fellaini aliingia uwanjani katika kipindi cha pili
cha mchezo ambao Man United walionekana kuutawala dhidi ya wachezaji 10 wa
Palace. Alifiti moja kwa moja kwenye kiungo cha kati ya timu hiyo, hakukosea na
akiwa uwanjani Man United walipata bao lao la pili.
Mbelgiji huyo alichukua nafasi ya Anderson, ambaye alionekana
kuchemka uwanjani, huku mashabiki wa Man United wakiomba Fellaini aingie, na
kuna kila dalili kwamba ataanza kwenye mechi dhidi ya Manchester City wiki
ijayo.
Christian
Eriksen (Tottenham)
Thamani:
Pauni milioni 11.5 (Sh bilioni 28.754)
Dakika
uwanjani: 71
Matokeo:
Tottenham 2-0 Norwich
Maksi:
8/10
Alichofanya
Christian Eriksen ambaye amesajiliwa kutoka Ajax ni
kiungo mshambuliaji mbunifu sana na alithibitisha hilo Jumamosi, kutokana na
kumpigia pasi maridadi ya mwisho Gylfi Sigurdsson ambaye alifunga bao la kwanza
kwenye mechi hiyo.
Japokuwa atakuja kuchukua namba ya Sigurdsson, pale
mastaa Aaron Lennon na Erik Lamela watakapokuwa fiti kuanza, juzi
alimtengenezea nafasi za kufunga, alionyesha kiwango kikubwa mpaka anatolewa
katika dakika ya 71.
Samuel
Eto'o (Chelsea)
Thamani:
Bure
Dakika
uwanjani: 90
Matokeo:
Everton 1-0 Chelsea
Maksi:
6/10
Alichofanya
Eto'o alitengenezewa nafasi kadhaa za kufunga,
lakini alikosa zote. Ya kwanza ilionekana kabisa kama ni bao, ila Gareth Barry
aliwahi na kuzuia shuti lake ambalo lilikuwa likielekea golini ambako hakukuwa
na mtu, aligongesha mwamba baada ya kupiga kichwa krosi iliyopigwa na Ramires.
Anaweza kujitetea kwamba bado hajawa fiti kucheza mechi za kiushindani.
Gareth
Barry (Everton)
Thamani:
Mkopo
Dakika
uwanjani: 90
Matokeo:
Everton 1-0 Chelsea
Maksi:
8/10
Alichofanya
Alikuwa na mechi nzuri kwenye eneo la kiungo.
Akicheza sambamba na Ross Barkley walishirikiana kuivunjavunja Chelsea na kitu mihumu
kuliko chote alichokifanya ni kuzuia shuti la Eto’o ambalo lilikuwa linaenda
golini, na kumnyima Mcameroon huyo bao la wazi.
Loic
Remy (Newcastle)
Thamani:
Mkopo
Dakika
uwanjani: 63
Matokeo:
Aston Villa 1-2 Newcastle
Maksi:
6/10
Alichofanya
Hakuonyesha kiwango cha kutisha sana kwenye mechi
hiyo na kujikuta akitolewa uwanjani katika dakika ya 63. Staa wa Newcastle
kwenye mechi hiyo alikuwa Hatem Ben Arfa, kama timu hiyo inataka kufanya vizuri
basi wanahitaji mabao kutoka kwa Papiss Cisse au Remy.
Thamani:
Pauni milioni 22 (Sh bilioni 55)
Dakika
uwanjani: 63
Matokeo:
Stoke 0-0 Man City
Maksi:
5/10
Alichofanya
Japokuwa hakusajili kwenye siku ya mwisho ya dirisha
la usajili, mechi hii ndiyo ilikuwa ya kwanza ya kimashindano kwake, na
hakuonyesha kiwango kizuri.
Alijaribu kuonyesha thamani yake, lakini mabeki wa
Stoke walimzuia asilete madhara na alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na
Sergio Aguero. Atafanya vizuri siku za usoni, lakini mechi ya juzi hakuwa yake
kabisa.
Marko
Arnautovic (Stoke)
Thamani:
Pauni milioni 2 (Sh bilioni 5)
Dakika
uwanjani: 20
Matokeo:
Stoke 0-0 Man City
Maksi:
7/10
Alichofanya
Marko Arnautovic anajulikana kwa jina la utani la
the Austrian Balotelli (Balotelli wa Austria), lakini jamaa huyo hakuonyesha
utata mwingi kwenye mechi dhidi ya Man City.
Alikaribia kufunga bao kwenye shuti la mwisho la
mechi, alipiga shuti ambalo lililopaa kidogo juu ya lango. Kabla ya hapo
alikaribia kulazimisha bao la kujifunga la Matija Nastasic.
Victor
Anichebe (West Brom)
Thamani:
Pauni milioni 6 (Sh bilioni 15)
Dakika
uwanjani: 78
Matokeo:
Fulham 1-1 West Brom
Maksi:
6/10
Alichofanya
Alicheza vizuri mbele akiwa mwenyewe, lakini umaliziaji
wake ulikuwa mbovu. Anichebe alishindwa kuvuma akiwa Everton, japokuwa alipewa
nafasi ya kuvuma, inawezekana akachemka na West Brom pia. Alicheza kiwango
kizuri, lakini hakuwa na jipya.
No comments:
Post a Comment