
TIMU ya Azam FC imerudi katika nafasi yake ya pili baada ya kuinyuka JKT Ruvu mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Chamanzi, jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Azam wamefikisha pointi 17 na kupanda hadi nafasi ya pili wakiwa na tofauti na pointi moja na vinara wa ligi hiyo, Simba wenye pointi 18 wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 15 katika nafasi ya tatu.
Mabao ya Azam yalifungwa na Humphrey Mieno, Erasto Nyoni na bao la tatu lilifungwa na Salum Aboubakar.
Katika michezo mingine iliyochezwa leo kwenye viwanja vingine vitatu ni kama ifuatavyo.
Mbeya City iliyopanda Ligi Kuu msimu huu imeendeleza makali yake katika ligi hiyo kwa kuibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dhidi ya wenyeji Mgambo Shooting, bao pekee la Jeremiah John dakika ya 20.
Mtibwa Sugar imefanya kufuru baada ya kuikung’uta mabao 5-2 JKT Oljoro Uwanja wa Manunu, Turiani mkoani Morogoro. Mabao ya Mtibwa yalifungwa na Juma Luizio dakika ya tano na 31 na Abdallah Juma matatu dakika ya 23, 66 na 78.
Juma aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea Simba SC msimu huu amefunga hat trick ya pili msimu huu baada ya Tambwe wa Simba SC, wakati mabao ya Oljoro yamefungwa na Shaibu Nayopa dakika ya 72 kwa penalti na Amir Omar dakika ya 84.
MTIBWA SUGAR 5 v 2 JKT OLJORO
RUVU SHOOTING 1v 0 RHINO RANGERS
MGAMBO SHOOTING 0 v 1 MBEYA CITY
No comments:
Post a Comment