BUKOBA SPORTS

Tuesday, October 15, 2013

DEBI YA DAR: KOCHA YANGA ERNIE BRANDTS KUMPANGA NGASSA JUMAPILI DHIDI YA SIMBA

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema ana imani kubwa mshambuliaji wake huyo atacheza katika kikosi cha kwanza katika mechi ya Jumapili dhidi ya Simba.
Ngassa atakuwa katika hali nzuri kama ilivyo kwa wachezaji wengine, tunajua kuwa amekuwa akifanya vizuri katika mechi zilizopita.

 Hivyo sina sababu ya kumuacha nje, hadi sasa hana tatizo lolote la kumfanya aukose mchezo huo.
Najua ni mechi ngumu, lakini tunachofanya ni kuangalia nini cha kufanya hasa tukipitia makosa katika mechi zilizopita.
Simba na Yanga zinakutana Jumapili katika mechi ya kwanza itakayozikutanisha msimu huu.

No comments:

Post a Comment