BUKOBA SPORTS

Sunday, October 6, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: SOUTHAMPTON 2 v SWANSEA CITY 0, RODRIQUES NA LALLANA WAIPANDISHA "TOP 4" SOUTHAMPTON!!

Southampton wakiwa kwao kwenye uwanja wa St. Mary's Stadium, mchezaji Midfielder Adam Lallana anaipatia bao timu yake dakika ya 19 kipindi cha kwanza. Hipindi cha kwanza pia Swansea wamepata nafasi na wameshindwa kuzitumia vyema huku Michu hakikosa bao la wazi. Kipindi cha kwanza kimemalizi Southampton wakiwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya Swansea City. Jay Rodriguez akitupia bao la pili.Mchezaji hatari wa wa Swansea Michu akijiuliza baada ya kukosa nafasi ya wazi kuipatia bao timu yake katika kipindi cha kwa kwanza. Kipa wa Southampton Artur Boruc akiruka kuokoa mpira golini kipindi cha pili.
Kipindi cha pili dakika ya 75 Southampton walipiga kona na mchezaji wa Southampton kufunga kona hiyo lakini mwamuzi wa pembeni akalikataa bao hilo.

Kipindi cha pili hicho hicho dakika ya 83 Mchezaji Jay Rodriguez aliweza kutumia udhaifu wa mabeki wa Swansea City na kuweza kupitiliza hadi kwenye mlango wao na kuweza kuiongezea timu yake ya Southampton bao jingine na kufanya 2-0 dhidi ya Norwich waliokuwa Ugenini. Ushindi huu wa Southampton unawapandisha hadi nafasi ya nne wakiwa na pointi 14 chini ya Chelsea waliofunga leo nao kufikisha pointi 14 wakitofautiana kwa magoli.
Wayne Routledge
 Wayne Routledge akimruka mchezaji Victor Wanyama wa Southampton

Swansea Southampton
Angel Rangel wa Swansea City akichuana na mchezaji wa  Southampton Steven Davis


Southampton's Pablo Daniel Osvaldo (left) is tackled by Swansea's Jordi Amat
Pablo Daniel Osvaldo kwenye patashika na Jordi Amat

Wilfried Bony
Wilfried Bonyakipiga kichwa hapa huku akiwa amenyemelewa na wachezaji wa Southampton

Michu
Umechelewa: Michu akibembea kwenye posti ya lango hapa
VIKOSI:
SOUTHAMPTON: Boruc, Clyne, Fonte, Lovren, Fox, Wanyama,
Schneiderlin, Lallana, Osvaldo
(Ward-Prowse), Steven Davis (Do Prado), Lambert (Rodriguez)
Subs not used: Davis, Cork, Chambers, Hooiveld
Booked: Fonte, Lovren, Wanyama
Scorer: Lallana, Rodriguez
SWANSEA: Vorm, Rangel, Amat, Chico, Ben Davies, Canas, Shelvey, Dyer, Michu, Routledge (Pozuelo), Bony
Subs not used: Taylor, Williams, Britton, Tiendalli, Tremmel, Vazquez
Booked: Canas
Att: 28570


RATIBA/MATOKEO
Jumapili October, 6
Norwich City 1 v 3 Chelsea
Southampton 2 v 0 Swansea City
18:00 West Bromwich Albion v Arsenal
18:00 Tottenham Hotspur v West Ham United

No comments:

Post a Comment