SERIKALI imesema leseni nyingi zinazotumika katika shughuli za utalii ni feki wengi wao wakiwa na simu za mikononi peke yake huku makazi na sehemu za kufanyia shughuli hizo kutokuwepo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema hayo jana Dar es salaam wakati akizundua bodi ya leseni ya bishara za utalii, mamlaka za rufaa wizarani hapo na Kamati ya ushauri.
Kuhusu leseni feki aliomba kupatiwa orodha ya wanaohusika na shughuli hizo kwani wengi wana leseni ambazo ni batili kutokana na utaratibu wa upatikanaji wake kutoeleweka.
“Katika wale wanaojishughulisha na biashara hiyo wengi wana simu za mikononi tu, huku makazi na sehemu za biashara kutokuwepo lakini wanapewa leseni,” alisema Balozi Kagasheki na kuongeza kuwa sekta hiyo ina umuhimu wa pekee na haijulikani wanazipateje leseni hizo na inaonesha wanapewa kinyume na utaratibu.
Aidha alisema serikali itaanza msako kuhusiana na hilo ili kuwe na njia za kudhibiti hao ambao huchukua mapato kinyume na utaratibu unaotakiwa ili kuziba mianya hiyo na kuifanya biashara ya utalii kuwa nzuri huku akiagiza Bodi zilizozinduliwa kushughulikia suala hilo ambalo hupoteza mapato mengi.
Akizungumza kuhusu masuala ambayo Bodi hizo zinapaswa kuyashughulikia kwa haraka alisema ni pamoja na kutizama kwa haraka suala la uboreshaji wa sera ya utalii ili kwamba iweze kuwa na sura y akitaifa na kimataifa kulingana na wakati uliopo.
“Ni vyema mkatizama sera imeekaje vilevile na sheria ya utalii ya mwaka 2008 kwani inaonekana kana kwamba wanasheria waliitunga kwa haraka haraha kutokana na kuwa na mikanganyiko mingi,” alisema Balozi Kagasheki.
Aidha alitoa mfano Makumbusho ya Taifa ambapo sheria yake ni ya mwaka 1980 ambapo hadi sasa hakuna kanuni jambo linalosababisha utekelezaji wa sheria hizo kutotelekezeka.
Alisema kutokana na hali hiyo ndio maana Bodi hizo zimekuwa na mchangayiko wa watu mbalimbali kutoka sekta binafsi ambao ni vyema kutumia busara zao na umakini ili kusaidia kutoa maamuzi ambayo ni ya msingi yenye kutizama maslahi ya Taifa.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi hizo wakifuatilia hotuba hiyo ya uzinduzi kutoka kwa Waziri.
Wajumbe wa bodi ya Leseni katika picha ya Waziri.
Wajumbe wa kamati ya Ushauri.
wajumbe wa Kamati ya rufani
Baadhi ya wajumbe wa Mamlaka ya Rufani, Crescencia Rwechungura (katikati), Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri, Dk. Wineaster Anderson pamoja na mjumbe wa bodi ya Leseni, Scholastica Ponera wakijadiliana jambo nje ya ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Utalii na Maliasili Dar es Salaam jana mara baada ya kuzindiliwa kwa bodi hizo.
No comments:
Post a Comment