
TIMU ya Taifa ya Zambia Chipolopolo ikiwa chini ya kocha wa mpito Patrice Beaumelle inashuka dimbani leo kukipiga dhidi ya mabingwa wa dunia mara tano Brazil kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa kwenye Uwanja wa Birds Nest.
Mabingwa hao wa zamani wa Africa watakuwa bila ya mshambuliaji Rodger Kola, Collins Mbesuma, kiungo Mukuka Mulenga na beki Davies Nkausu ambao ni majeruhi.
Pia wachezaji Nathan Sinkala, Stopilla Sunzu, Rainford Kalaba wameshindwa kuripoti kwa wakati kwenye maandalizi ya mchezo huo.
Nahodha Christopher Katongo, Noah Chivuta, Chisamba Lungu na Fwayo Tembo wapo kamili kuitumikia Zambia kwenye mchezo huo ambapo Jacob Mulenga kuongoza mashambulizi na James Chamanga huku Emmanuel Mayuka likiwa ni chaguo lingine.
Brazil kwa upande wao watakuwa bila ya kipa Julio Cesar, beki Thiago Silva na mshambuliaji Fred.

Felipe Luiz Scolari anatarajia kufanya mabadiliko kadhaa Diego Cavalieri atambadili Jefferson langoni wakati Daniel Alves, Dedé, David Luiz na Maxwell watatengeneza ukuta.
Lucas Leiva, Paulinho na Ramires wanatarajiwa kuanza kwenye kiungo huku Lucas, Alexandre Pato na Jo wakiwa kwenye ushambuliaji.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana
No comments:
Post a Comment