BUKOBA SPORTS

Thursday, October 10, 2013

KWA MAZOEZI HAYA KAGERA SUGAR MJIANDAE KWA KIPIGO!!! UTEJA UTAISHIA HAPA!! WACHEZAJI WA YANGA WAKIFANYA MAZOEZI KATIKA UWANJA WA NTUNGAMO NJE KIDOGO YA MJI WA BUKOBA, TAYARI KWA MPAMBANO NA KAGERA SUGAR JUMAMOSI KAITABA.


Timu ya yanga wakiomba dua kabla ya mazoezi kuanza katika uwanja wa ntungamo seminary. www.bukobasports.com
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Young Africas leo jioni wamefanya mazoezi katika viwanja vya shule ya seminari ya wakatoriki Ntungamo - Kashura pembeni kidogo ya mji wa Bukoba kujiandaa na mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba.

Kelvin Yondani aliyeripotiwa na chombo kimoja cha habari kwamba ameondolewa kwenye timu taarifa hizo hazina ukweli kwani mlinzi huyo kisiki wa kati ni miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi jioni ya leo pamoja na kikosi cha Yanga.

Young Africans ambayo iliwasili katika mji wa Bukoba majira ya saa 5 asubhi ikitokea jijini Dar es salaam ambapo ilipitia jijini Mwanza kabla ya kutua kwenye mji huu ambao una mandhari mazuri na hali ya hewa safi.

Kocha mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts ametumia muda wa masaa mawili kuwafua vijana wake 21 ili kuwa fit kuelekea mchezo huo wa jumamosi ambao ni muhimu kwa Yanga kupata pointi 3 ili kujiweka katika mazingira mazuri.

Timu ilipolekelea uwanja wa ndege na umati mkubwa wa wapenzi na washabiki wa Yanga ambao walisema wamefurahia kuiona timu yao tena ikiwa katika mji huu na kusema watashilikiana bega kwa bega kuhakikisha timu inapata pointi 3 kwenye mchezo huo.

Kesho jioni Young Africans itafanya mazoezi katika uwanja wa Kaitaba yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo wa siku ya jumamosi.

Wachezaji waliofanya mazoezi leo jioni ni:
Walinda Mlango: Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul

Walinzi : Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', na Kelvin Yondani

Viungo: Haruna Niyonzima, Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo, Nizar Khalfani, Mrisho Ngassa na Saimon Msuva

Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerson Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi na Abdallah Mguhi 'Messi'


Vijana mazoezini
Ni kuruka juu na kushuka
Uwanja wa ntungamo si mchezo
Kocha mkuu wa Yanga kazini
Eheee sitaki mchezo hapa

Mazoezi kwa vitendo
Kipa akiwa katika mazoezi ya viungo

Kocha mkuu na msaidizi wakifuatilia mazoezi

Mazoezi ya viungo

Vijana wako kikazi zaidi point tatu ndio sera waliyonayoMeneja wa Yanga akibadilishana mawazo na wadau katika mazoezi
Kushoto msemaji wa Yanga akifuatilia mazoezi
Wadau jamco kushoto,ninyonzima na Haruna kabla ya mazoezi kuanza, JUMAMOSI ITAKUWA BALAA!! ...NI JUMAMOSI KUBWA!

No comments:

Post a Comment