MASHAUZI KUTAMBULISHA MPYA IDD EL HAJJ Da' WEST TABATA KESHO JUMATANO
Bendi ya taarabu ya Mashauzi Classic kesho (Jumatano) itatambulisha nyimbo zao mpya kwenye onyesho maalum ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Hajj katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata.Onyesho hilo ambalo linajulikana kama ‘Usiku wa Isha Mashauzi’, imeandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment chini ya udhamini wa kinywaji cha Konyagi, Straika, Kwetu Mbambabay na Saluti5. Mratibu wa onyesho hilo, Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho litakuwa la kipekee na maalum kwa kusherehekea sikukuu ya Idd El Hajj. Amesema katika onyesho hilo, Mashauzi atatambulisha albamu yake mpya.
No comments:
Post a Comment