MCHEZAJI wa Uingereza ambae si mgeni wa vituko, matukio na vurugu katika maisha yake, Joey Barton, ameibuka na kubatuka Lejendari Sir Alex Ferguson hakuwa na uwezo wa kufundisha Timu.
Barton aliongelea kuhusu Ferguson wakati akichangia mada ya jinsi ya kuongeza Wachezaji wenye Asili ya Kiingereza kuchezea Ligi Kuu England mara tu baada ya Mwenyekiti wa FA ya England, Greg Dyke, kuteua Kamisheni kushughulikia suala hilo baada utafiti kubani ni Asilimia 30 tu ya Wachezaji wa Ligi hiyo ni Waingereza.Sir Alex Ferguson alistaafu kuwa Meneja wa Man United Mwezi Mei baada ya kuiongoza Klabu hiyo kwa Miaka 26 na Nusu na kushinda Mashindano 38 ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu England mara 13, Ubingwa wa Ulaya mara 2 na Ubingwa Klabu Duniani mara 2.
Barton kushoto....
Klabu ya QPR imemvua Unahodha Joey Barton na kumtwanga Faini ya Mishahara ya Wiki 6 na pia kumpa onyo kuwa akirudia kosa Mkataba wake utafutwa kufuatia kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England walipocheza Uwanja wa Etihad na Manchester City Mwezi Mei.Mbali ya adhabu hii ya Klabu yake, Chama cha Soka England, FA, tayari kilishatoa adhabu kwake kwa matukio hayo ya huko Etihad kwa kumtwanga Faini ya Pauni 75,000 na kumfungia Mechi 12 kwa sababu ni Mkosaji alierudia makosa yake.
Adhabu zote hizi kwa Joey Barton zitamgharimu Pauni 500,000 lakini mwenyewe, mbali ya kukubali makosa yote, amekiri si Pesa ambazo zitamuumiza bali ni kupoteza Unahodha na kukosa kuichezea QPR Mechi 12 Msimu ujao utakapoanza.
No comments:
Post a Comment