Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah (kulia) akionyesha fomu za kujiunga na Tamasha la Mitindo kwa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini lijulikanalo kama Redd's Uni-Fashion Bash kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi Tamasha hilo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Kampuni hiyo,Edith Mushi.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Edith Mushi (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za Washindi mbali mbali Watakaoshiriki kwenye Tamasha la Mitindo kwa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini lijulikanalo kama Redd's Uni-Fashion Bash.Tamasha hilo limezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Fimbo Butallah
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza Uzinduzi wa Tamasha la Mitindo kwa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini lijulikanalo kama Redd's Uni-Fashion Bash.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imezindua tamasha la aina yake la mitindo kwa vyuo vya elimu ya juu. Tamasha hili litakalojulikana kama “Redd’s Uni-Fashion Bash” kwa mwaka huu litaanza mwezi huu wa Octoba hadi Novemba na kushirikisha vyuo vyote vya elimu ya juu vilivyo katika mikoa minne ambayo ni Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Iringa na Mwanza.
Akizungumza katika uzinduzi huo, meneja Masoko wa Tbl Fimbo Buttalah alisema; “Tamasha hili la mitindo lina lengo la kuinua vipaji vya wanafunzi wa vyuo katika tasnia ya mitindo kupitia maonesho yatakayofanywa katika vyuo, ambapo wanafunzi wenye vipaji vya ubunifu watapata fursa ya kuonesha ubunifu wao wa mitindo. Hii ni fursa kubwa kwao kujitangaza na kudhihirisha uwezo wao.”
Bwana Fimbo, pia alielezea utaratibu wote wa kuwapata wabunifu watakaoonesha kazi zao jukwaani wakati wa matamasha haya ya aina yake kwa kusema; “Uzinduzi huu utafuatiwa na usajili wa wanafunzi wabunifu na wanamitindo kupitia fomu maalum zitakazosambazwa vyuoni, kisha majaji watachambua fomu zote zilizowasilishwa na kupata wabunifu 10 katika kila mkoa watakaokidhi vigezo, ambao watapata fursa ya kuonesha mavazi yao siku ya tamasha, pia kutakuwa na nafasi 10 kwa wanamitindo watakaovaa mavazi hayo jukwaani. Majaji wataangalia vigezo na kupata washindi ambao watapata zawadi toka kwa kinywaji cha Redd’s Original.”
Akizungumzia zawadi kwa washindi, meneja mawasiliano na Habari wa Tbl Edith Mushi alisema; Zaidi ya kuwapatia jukwaa wabunifu na wanamitindo hawa ili waweze kuonesha vipaji vyao, Redd’s pia itawapatia zawadi za pesa washindi watano katika kila mkoa watakaoshika nafasi za juu kama ifuatavyo;
Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu kwa wabunifu kujidhatiti katika kuendeleza ubunifu katika tasnia hii ya mitindo. Lakini pia matamasha haya yatahusisha burudani mbalimbali za kuvutia na hivyo kuwa sehemu muhimu ya kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo na kada mbalimbali katika kufurahia na kubadilishana mawazo juu ya masuala ya ubunifu na mitindo.
Kinywaji cha Redd’s Original kimekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza tasnia ya urembo, ubunifu na mitindo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment