Refa East, ambae Msimu huu ndio amepandishwa na kuingizwa Kundi la Marefa wanaochezesha Ligi Kuu, alimuudhi sana Meneja wa Stoke Mark Hughes kwenye Mechi hiyo na Fulham kwa kutoa maamuzi yenye utata ikiwa ni pamoja na kushindwa kumpa Kadi Nyekundu Mchezaji wa Fulham Pajtim Kasami kwa kumpiga Erik Pieters.
Mara baada ya Mechi hiyo Mtendaji Mkuu Tony Scholes alimpigia Simu Mike Riley ambae ndie Mkuu wa PGMOB, Professional Game Match Officials Board, Bodi ya Marefa.
Refa East Wikiendi hii hakupangiwa Mechi yeyote ya Ligi Kuu na Msimu huu amechezesha Mechi mbili tu za Ligi Kuu.
Referee Roger East, Stoke’s 1-0 defeat by Fulham
No comments:
Post a Comment