TIMU ya Taifa ya wasichana waliochini ya miaka 20, jana ilipokea kichapo cha mabao 3-1 toka kwa timu ya wavulana ya Karume Kombaini ya U-16 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa kutafuta kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Msumbiji utakaochezwa Oktoba 26 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko lakini kombaini ndio walionufaika baada ya kuongeza mabao mawili yaliyofungwa na Abdul Biteko katika dakika ya 70 na 81 na kufanya matokeo kuwa 3-1.
Pamoja na kufungwa timu ya taifa ya wasichana walicheza mchezo mzuri na wa kuvutia na kuwapa matumaini mashabiki waliofurika uwanja hapo kufanya vizuri katika michezo yao ya kutafuta kufuzu Kombe la Dunia.
“Timu yangu imecheza vizuri na naamini itafanya vema katika mashindano yanayotukabili pia nawaomba watanzania watupe sapoti kwa kufika kwa wingi uwanjani kutushangilia”, alisema Kaijage.
Fainali za Dunia za U-20 kwa wanawake zitafanyika mwakani nchini Canada. Iwapo Tanzania itaitoa Msumbiji katika raundi hii, raundi inayofuata itacheza na mshindi kati ya Botswana na Zimbabwe na ikifanikiwa kupita Tanzania itashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya Kombe la Dunia kwa wasichana.
No comments:
Post a Comment